NYUKI MKOMBOZI KIUCHUMI
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/29-11-2013/10:41
Taasisi wa
masuala ya haki za binadamu na maendeleo WAHABIMA wanuia kusaidia wajasiriamali
wa mjini wa Kibaha katika suala zima la ufugaji wa nyuki wa asali ili kuongeza
kipato cha familia.
Akizungumza
katika uzinduzi wa warsha inayohusiana na ufugaji nyuki wa asali, Mshauri
mwelekezi, BW.DOMINIC KIWELE amewaeleza washiriki kuwa ufugaji wa nyuki
ukifanywa kwa kuzingatia ushauri wa kitaalamu unaweza kukikomboa familia na umaskini wa kipato
ambao ndio tatizo kubwa miongoni mwetu.
BW.KIWELE
amebainisha kuwa gharama za kuanzisha ufugaji wa nyuki ni ndogo kulinganisha na
ufugaji mwingine wowote kwani ili kuweza kufuga nyuki itakubidi kuingia gharama
kidogo kwa ajili ya kutengenezea mzinga ambao utatumika kutegea nyuki ukiwa na
chambo chake ambacho ni nta inayozalishwa na nyuki.
Mshauri
mwelekezi huyo, BW.DOMINIC KIWELE amefafanua kuwa watu wengi wamekuwa wanaogopa
kufuga nyuki wakihofiwa kushambuliwa nao kitu ambacho sio loazima na hasa
ukizingatia unafuga nyuki wa aina gani, kwani kuna aina mbili za nyuki, moja ni
nyuki wanaouma qambao inashauriwa kuwafuga mbali na jamii na aina ya pili ni
nyuki wasioouma maarufu kama nyuki wadogo hao wanaweza kufuga karibu na jamii.
Naye ofisa
wa maendeleo ya jamii halmashauri ya mji wa Kibaha BI.LEAH LWANJI amepongeza hatua
iliyofanywa na WAHABIMA kuwafikia
wakazi wa eneo la Miswe chini katika kuwawezesha kutambua umuhimu wa ufugaji wa
nyuki katika suala zima la familia kujiongezea kipato.
BI.LWANJI
amewataka watendaji katika halmashauri kutoa ushirikiano wa hali na mali kwa
taasisi hiyo yenye lengo la kumkomboa mwananchi kiuchumi kupitia ufugaji wa
nyuki.
END.
Comments
Post a Comment