WAFUGAJI WAILILIa SERIKALI
Ben
Komba/PWANI-TANZANIA/11/7/2013 9:33:09 AM
Wafugaji
nchini wamemtaka Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DKT.JAKAYA KIKWETE wabebe
dhamana juu ya watu waliokufa kufuatia mapigano kati ya ushiriki unaosimamia
masuala ya maliasili na uhifadhi wa misitu ya MWANU.
Akizungumza na
mwandishi wa habari hizi, Katibu wa wafugaji Tanzania BW.GEORGE KIFUKO amesema
tatizo hilo linasababishwa na viongozi wa mkoa wa Morogoro kutokana na
uanzishaji wa kamati ambayo inatekeleza operesheni ya kukamata mifugo.
BW. KIFUKO
amesema kuwa Mkuu wa wilaya ya Mvomero ndio ameanzisha zoezi hilo kwa maslahi
binafsi kwa kukamata ng’ombe na kuwalazimisha wafugaji kulipa shilingo milioni
10 ili kuweza kukomboa ng’ombe hao takriban 300, Jambo ambalo wafugaji
hawajakubaliana nalo na kutaka waende mahakamani kwa hatua zaidi jambo ambalo wakamataji hao wa mifugo
walikataa.
Amemtaka Rais
KIKWETE afikie hatua achukue maamuzi ya kuzuia unyang’anyi wa mali za wananchi,
mauaji na kila aina uvunjaji wa katiba ya wananchi na hasa kwa kuzingatia hakua
ambaye yupo juu ya sheria.
Naye mfugaji
BW.SIMON FAHAMUHERI ambaye ni mkazi wa kijiji cha Kambala Kata ya Mbiki
wilayani Mvomero amemwambia mwandishi wa habari hizi kuwa juzi watu wa MWANU
walikwenda kukamata ng’ombe katika eneo la mfugaji na huku wakiwalazimisha
wafugaji watoe kiasi cha shilingi Milioni 10.
END.
Comments
Post a Comment