WANANCHI PWANI WASHAURIWA KUTHAMINI ELIMU



Ben Komba/Pwani-Tanzania/24-11-2013.
Wananchi Mkoa wa Pwani wametakiwa kutumia fursa ya kupata elimu kutokana nauwepo wa taasisi za kutoa elimu katika suala zima la kuhakikisha kila mwananchi mwenye uwezo na kujitambua anapata elimu ambayo itaweza kumsaidia maishani.

Akizungumza katika mahafali ya nane ya Chuo cha Ufundi Masakamali kilichopo Msata wilayani Bagamoyo katika mkoa wa Pwani, Mkaguzi msaidizi wa Polisi usalama Barabarani wilaya ya Bagamoyo, INNOCENT SULLE amewataka wazazi kuhakikisha kuwa wanawapeleka watoto wao shule ili waweze kuja kuwasaidia na kujisaidia maishani.

BW.SULLE amewaambia wanafunzi hao wahitimu kutokubali kuishia hapo walipofikia na kuwataka wajiongeze ili kupiga hatua kubwa katika masomo kwa kujiunga na vyuo vingine vyenye kutoa tunzo za juu zaidi.

Mkaguzi huyo wa usalama barabarani ametoa mfano wa waendesha bodaboda wa Msata ambao wengi wao hawana leseni ya kuendesha chombo hicho cha moto pamoja na uwepo wa karibu wa chuo cha ufundi Msakamali ambacho pia kinatoa mafunzo ya udereva.

Aidha BW.SULLE ametumia fursa hiyo kuwahimiza waendesha Bodaboda kuhakikisha wanapata mafunzo ya kuendesha pikipiki na yoyote ambaye atapuza atakumbwa na mkono wa sheria kutokana na wao sasa kukosa sababu ya kukosa leseni toka elimu hiyo kwa sasa inapatikana karibu na mazingira yao.

Naye mkuu wa chuo cha ufundi Msakamali, BW.BARNABAS MLWILO amesma chuo hicho kimeanzishwa mwaka2006,kikiwa na lengo la kuwapatia elimu ya ufundi stadi kwawanafunzi ambao wameshindwa kwenda Sekondari.

BW.MLWILO amebainisha kuwa chuo kinajishughulisha na ufungaji wa Kondoo, Punda, Kuku na uoteshaji wa miti mbalimbali, ikiwa na utoaji wa kozi ndefu na kozi ndefu kwa wanafunzi wanaojiunga nacho.

END.

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA