Ben Komba/
Taasisi isiyo ya kiserikali ya MBONDE FOUNDATION inayoshughulika na watoto wanaoishi katika mazingira magumu na yatima imetoa vifaa vya shule kwa wanafunzi zaidi ya 40 wa shule ya msingi Boko Timiza,halmshauri ya mji wa Kibaha katika suala zima la utekelezaji wa shughuli za kijamii.
Msemaji wa Taasisi ya MBONDE FOUNDATION yenye maskani yake mjini Dar es Saalam, BW. WILSON EZEKIEL amesema msaada huo kwa watoto ambao ni viatu, madaftari, Kalamu na Peni ni mwanzo wa usaidizi kwa watoto hao mpaka watakapofikia elimu ya sekondari.
BW.EZEKIEL ameongeza watoto hao ambao kila mmoja amepatiwa namba maalum ya utambulisho na tayari wameshatengewa bajeti ya mwaka mzima kwa ajili ya mahitaji yao muhimu ya shule.
Mmoja wa wanafunzi ambao wamefaidika na msaada huo ameishukuru taasisi hiyo kwa kuwapatia msaada huo ambao utawasaidia kufanya vizuri katika masomo yao na halikadhalika wamewasaidia wazazi wao kwa kiasi Fulani katika kuwapunguzia majukumu.
Naye mmoja wa wazazi wa watoto hao ameishukuru taasisi hiyo ambayo wakati wa ujio wake kulisikika maneno chungu mzima kwa kudai watu hao ni matapeli na wengine walifika mbali zaidi na kuwaita FREEMASON kitu ambacho kwa sasa kimedhihirika sio kweli.
Na amewataka kuendelea na usaidizi wao kwa watoto wenye uhitaji ili kuweza kuongeza kasi ya mafanikio katika sekta ya elimu.
END.
Comments
Post a Comment