MAJANGA YA AJALI BARABARANI.
SIKU YA MAJANGA YA AJALI ZA BARABANI
Ben Komba/Pwani-Tanzania/26-11-2013/10:35
Katika maadhimisho ya siku ya majanga ya ajali za barabarani ulimwenguni ambayo inafanyika kila jumapili ya tatu ya mwezi wa Novemba ya kila mwaka na nchi mbalimbali zimekuwa zinaadhimisha siku hiyo na mwaka huu maadhimisho hayo kitaifa yamefanyika mjini Kibaha katika mkoa wa Pwani.
Akizungumza katika maadhimisho hayo Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani nchini, Kamishna msaidizi MOHAMED MPINGA amesema ikumbukwe kuwa ajali za barabarani ni janga la kiulimwengu katika sekta ya afya, na zinachangia kiasi cha vifo vya watu milioni 100.3 kwa mwaka na kusababisha majeruhi watu milioni 20 mpaka milioni 50 kwa mwaka.
Kamanda MPINGA amebainisha ajali za barabarani zinashika nafasi ya nane kwa kusababisha vifo kilimwengu,na kama hatua madhubuti hazitachukuliwa kama tafiti zinavyoonyesha mpaka mwaka 2020 kuna uwezekano mkubwa wa ajali kushika namba tano kuwa ndio chanzo kikubwa kinachosababisha ajali ulimwenguni.
Kamanda MPINGA ameongeza kuwa takwimu zinaonyesha kwamba kwa mwaka huu pekee kumetokea ajali hadi Oktoba 2013, ajali 19939 zilitokea na watu waliofariki 3285 na waliojeruhiwa ni watu 17311, hii haiusishi ajali zilizotokea hivi karibuni kama iliyotokea mkoani Morogoro Wami sokoine kulitokea ajali ambayo iliua watu saba baada ya NOAH kugongana na Lori la mizigo.
Aidha amesisitiza kuwa hali hiyo haiwezi kuvumilika na hasa kutokana na ajali kusababisha vifo ambavyo kwa njia moja au nyingine ni nguvu kazi na wengi wanaopoteza maisha wengi wao wakiwa vijana kati ya miaka 18 mpaka 35, amezungumzia pia suala la ajali wanazopata wanafunzi wanapoenda na kurudi mashuleni.
Kamanda huyo wa Kikosi cha usalama barabarani, Kamishna msaidizi MPINGA amefafanua katika kupunguza ajali za barabarani zinazohusisha wanafunzi hatua mbalimbali zimeanza kuchukuliwa kwa kuanzisha utaratibu wa Junior Patrol inayohusisha wanafunzi watakaopatiwa mafunzo maalum na ambao watapatiwa vikoti vinavyoakisi mwanga au REFLECTOR watakazotumia kuvushia wanafunzi wenzao.
Akiongea katika maadhimisho ya siku hiyo, Mkurugenzi wa taasisi isiyo ya kiserikali ya HELMET VACCINE INITIATIVE TANZANIA ambayo kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani, BW. ALPHERIO NCHIMBI amesema siku hii ni maalum kwa ajili ya kuwakumbuka mamilioni ya wahanga wa ajali za barabarani ambao wamepoteza maisha na kujeruhiwa.
BW.NCHIMBI ameongeza kuwa siku hii pia inatumika kuwashukuru wato huduma wote wa sekta ya afuya kwa kuwa begabega inapotokea ajali zinazosababisha majeruhi na vifo.
END.

Comments
Post a Comment