WAZAZI WATAKIWA KUSAIDIANA WALIMU
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/17-09-2013/10:22
Wazazi
nchini wametakiwa kusaidiana na Walimu katika kuhakikisha wanafunzi wanapata
mafanikio ya kielimu na kijamii ili kuweza kujenga jamii yenye maarifa na
nidhamu ambayo itawasaidia katika maisha yao ya baadaye.
Akizungumza katika
mahafali ya kumaliza elimu ya msingi Katika shule ya KIBAHA INDEPENDENT mjini
Kibaha, Mke wa Mbunge wa Jimbo la uchaguzi Kibaha mjini, BIbi.SELINA KOKA
amewaasa wazazi kutowaachia Walimu pekee jukumu la kuwalea watoto kielimu.
BIBI.KOKA
amefafanua kutokana na wakati mwingi wanafunzi kuwa Walimu katika suala zima la
kupatiwa elimu na ulezi wanapokuwa shuleni, na wazazi nao hawana budi
kuwajibika katika kuhakikisha mara mwanafunzi anaporudi kutoka shule wanangalia
maendeleo yao katika kuhakikisha malengo ya kuwapatia wanafunzi elimu bora
yanafikiwa.
Aidha BIBI.KOKA
ameutaka uongozi wa shule hiyo kuingiza masomo ya upishi na kudarizi katika
silabasi yao katika kuhakikisha wanapanua wigo wa utoaji elimu katika taaluma
mbalimbali ili kutoa fursa kwa wanafunzi kuwa na chaguo zaidi ya moja
wanapotaka kuendelea na masomo ya elimu ya juu.
Naye mkuu wa
shule ya KIBAHA INDEPENDENT, BW. HEZRON MSALALE amesema ndoto ya shule yake ni
kutoa elimu bora ya awali, Msingi na sekondari ya Kiwango sthahili ili kuwaanda
vijana katika kuwa maarifa na stadi za hali ya juu zinazohitajika kutanzua
changamoto mbali zinazokabili jamii yetu.
END.
Comments
Post a Comment