MAMLAKA YA HALI YA HEWA WAKUTANA NA WAHARIRI



Ben Komba/Pwani-Tanzania/04-09-2013/16:26
Mkuu wa mkoa wa Pwani BIBI. MWANTUMU MAHIZA ameitaka mamlaka ya hali ya hewa nchini kuvitumia vyombo vya habari kwa makini ili viweze kusaidia wananchi kuelewa umuhimu wa mamlaka hiyo katika utekelezaji wao wa majukumu ya kila siku.

Akiongea katika semina ambayo imewahusu wahariri wa vyombo vya habari nchini iliyoandaliwa na mamlaka ya hali ya hewa, BIBI. MAHIZA amesema baadhi ya wananchi wengi wananchi wengi wa nchi yetu wanajifanya hamnazo kwa kupuuza taarifa inayotolewa na mamlaka ya hali ya hewa.

Ameishauri mamlaka ya hali ya hewa kuweka sheria zitakazowabana wananchi ambao watapuuza maelekezo yanayotolewa na mamlaka ya hali ya hewa, kama mamlaka inatangaza bahari imechafuka lakini kuna baadhi yao wanaingiza vyombo baharini na matokeo ya karibuni yalisababisha vifo vya watu 18.

BIBI. MAHIZA amesema kutokana na upuuzi hali imekuwa mbaya zaidi na wakati mwingine kusababisha majanga, ameishauri mamlaka hiyokupeleka muswada bungeni kuwabana watu wote wasiozingatia ushauri wa mamalaka hiyo.

Naye Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya hali ya hewa, BIBI.AGNES KIJAZI amevishukuru vyombo vya habari kwa kutoa taarifa mbalimbali zinazotolewa na mamlaka hiyo kama mvua kubwa, upepo mkali, lakini kuna changamoto zimejitokeza kama lugha inayotumika kutoeleweka vizuri na wakati mwingine kutolewa kwa taarifa potofu.

BIBI.KIJAZI amebainisha kuwa ili kukabiliana na changamoto hizo mamalaka imeandaa semina kwa waandishi wa vyombo vya habari ili kuwawezesha kuripoti habari zinazohusiana na kwa weledi.

END.

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA