ULINZI SHIRIKISHI JAMII.

ULINZI SHIRIKISHI JAMII.

Ben Komba/14-09-2013/12:11

Katika hali inayoonyesha wananchi wameanza kupata mwamko kuhusiana na suala zima la ulinzi shirikishi, vijana waendesha bodaboda mjini Kibaha wakitumia mbinu za Polisi jamii wamefanikiwa kumkamata kijana anayetuhumiwa kujihusisha na vitendo vya kiuhalifu dhidi ya madereva wenzake na abiria.

Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi ya waendesha Bodaboda mjini hapa BW.JOHN JOSHUA, Amesema kutokana na kuwepo kwa malalamiko kutoka kwa wateja na madereva wenzie kuhusiana na Kijana aliyekamatwa BW.SIFAEL BOLEGOLE  aka MWIBA ambaye ana makazi katika maeneo ya Kibaha-Nyumbu na Kimara.

BW.JOSHUA amebainisha kuwa siku moja BW.SIFAEL BOLEGOLE aliufikia uongozi na kuwataarifu kuwa kuna mtu amemwendea na kumpa mpango wa wizi wa pikipiki, kitu ambacho binafsi alikuwa hajafurahishwa nacho, na ndipo wakamwelekeza mtuhumiwa kwenda kwa Aliyempa mpango huo ambaye ni BW.SEIF na kujifanya kukubaliana naye.

Mwenyekiti huyo wa Kamati ya ulinzi ya waendesha bodaboda mjini Kibaha BW.JOHN JOSHUA ameongeza kuwa mara baada ya kupanga mpango huo walifanikiwa kumkamata mwizi huyo wa pikipiki BW.SEIF akiwa anatekeleza uhalifu huo.

Lakini mara baada ya BW.SEIF kukamatwa wakati wa kuhojiwa alimtaja BW. SIFAEL BOLEGOLE aka MWIBA kuwa walikuwa wanashirikiana naye katika utekelezaji wa matukio mbalimbali ya kihalifu na ndipo hatua za kumkamata zikafanyika na kumfikisha katika kituo kidogo cha Polisi Maili moja.

Naye Afisa wa operesheni wa ulinzi na usalama mkoa wa Pwani BW.PETER MADAHA amesema kuna mikakati ya kudhibiti madereva wanaofanya vitendo visivyo vya kistaarabu kwa wateja na madereva wenzao kwa kuweka kanuni ambazo zitawezesha kuwafukuza madereva wote wanaokwenda kinyume na maadili ya kibinadamu.
END.

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA