USHIRIKA WAHUJUMIWA

USHIRKA WAHUJUMIWA

Ben Komba/Pwani-Tanzania/Thursday, September 12, 2013

Wanachama wa chama cha ushirika cha wakulima wa umwagiliaji mpunga Bonde la Mto Ruvu juu CHAURU wilayani Bagamoyo,wameulalamikia uongozi wa ushirika huo kwa kufanya mambo kinyume na taratibu za ushirika.


Akiongea na mmoja wa wanachama wa siku nyingi wa Ushirika huo, BW.SADALLAH CHACHA mwanacham namba,1.12.2 amebainisha  kuwepo ubadhirifu wa mali za ushirika kwa manufaa binafsi.


BW.CHACHA  amesema anashudia kuona ushirika ukiendeshwa bila kufuata kanuni na taratibu zilizowekwa kupitia katiba ya ushirika huo, amebainisha katika mambo ambayo wanachama hawakubaliani nayo ni pamoja na uwepo wa Wachina bila kushirikisha wanachama.


Ametoa mfano wa ghala lililokuwa linatumika kuhifadhi mazao ya wanachama wa ushirika huo ambalo Mwenyekiti wa ushirika huo, BW.ZAHOR SENG’ENGE amewakabidhi wachina ambao wamejenga uzio ili kuwanyima fursa wanachama wa ushirika kutumia.


Bw.CHACHA amefafanua na mara zote wakitaka kujua kuhusiana na uwepo wa wachina hao eneo hilo, wamekuwa wakitishwa na Mwenyekiti wa ushirika kwa kuwaambia kuwa wao wana njama ya kuwavamia wawekezaji hao ambao hawatambuliki rasmi na wanachama.


Akijibu tuhuma hizo Mwenyekiti wa ushirika huo, BW.ZAHOR SENG’ENGE amekanusha madai hayo kwa kusema siyo ya kweli na wanaofanya hivyo hawautakii mema ushirika huo.


BW.SENG’ENGE amebainisha kuwa wengi wao hawajui malengo ya kuendesha ushirika na kuleta matokeo makubwa sasa, na ameongeza kuwa yeye ataendelea na mipango ambayo ushirika umejiwekea ili kuboresha mazingira ya kilimo katia ushirika huo.

Naye Ofisa ushirika wilaya ya Bagamoyo, BW.AHMED BUMBO kutaka kujua kama ana taarifa zozote kuhusiana na mgogoro huo, yeye amekanusha juu ya kupata taarifa zozote kuhusiana na uwepo wa mgogoro katika ushirika wa CHAURU.

END.

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA