VIKWAZO VYAMKWAMISHA MWEKEZAJI SEKTA YA SUKARI

ECOENERGY YAOMBA KUONDOLEWA VIKWAZO.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/13-09-2013/09:50
Waziri wa nchi ofisi ya Waziri mkuu uwekezaji na uwezeshaji, BIBI.MARY NAGU amesema serikali itahakikisha inaondoa vikwazo vinavyokabili wawekezaji katika sekta ya sukari ili waweze kupata tija wao na ustawi wa uchumi.

Ameyasema hayo kufuatia ziara ambayo ameifanya kutembelea mradi wa shamba la mwekezaji ECOENERGY katika eneo la Gama wilayani Bagamoyo, ambapo Waziri NAGU amesema vikwazo vya upatikanaji wa vibali vya umiliki wa ardhi vinaondolewa.

Waziri NAGU amesema lengo la kwenda kuzuru eneo hilo ni kutaka kuhakikisha ECOENERGY wamefikia wapi ili waweze kuogeza kasi ya ukamilishaji wa mradi huo na ikizingatiwa Tanzania ina upungufu mkubwa wa sukari na hivyo kwa kutumia wawekezaji tatizo hilo linaweza kukabiliwa.

Mwenyekiti mtendaji wa ECOENERGY, BW.PER CUSTERED amemueleza Waziri NAGU kuhusu changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo toka wameanza mradi huo ambao ulianza rasmi mwaka 2006, lakini mpaka leo wamekuwa wakikabiliwa na vikwazo ambavyo vinarudisha nyuma maendeleo ya Mradi.

Mbali ya kutoa maelezo kwa Waziri wa uwekezaji na uwezeshaji BIBI.MARY NAGU, Mwenyekiti mtendaji wa ECOENERGY, BW.CUSTERED alimtembeza katika shamba hilo kuona shughuli za uzalishaji pamoja kituo cha uzalishaji wa umeme unaosaidia katika uendeshaji mzima wa mradi.END

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA