TEMBEA KWA AJILI YA TEMBO
TEMBEA KWA AJILI YA TEMBO.
Ben Komba/Pwani-Tanzania/12-09-2013/02:12
Wanaharakati wa kupinga ujangili kutoka Arusha ambao umeshika kasi nchini wamefanya matembezi kuiamsha jamii kuamka kifikra kwa kujua jukumu la kulinda maliasili zetu ni jukumu la kila mtu.
Kiongozi wa wanaharakati hao BW.MKAZENI MKAZENI amesama wao wanafanyakazi na AFRICAN WILDLIFE TRUST yenye maskani yake Arusha ambayo moja ya malengo yake makuu na kupambana na wawindaji haramu.
BW.MKAZENI amesema safari yao wameianza tarehe 24 Agosti na kupewa Baraka zote na Mkuu wa Arusha, BW.MAGESA MULONGO na kupata ushirikiano mkubwa kutoka kwa watu mbalimbali walipokuwa katika matembezi hayo, na amesisistiza hawana itakadi za chama chochote cha siasa.
Naye mmoja wa washiriki wa matembezi hayo bibi.REHEMA MSUYA amesema kwa upande wake yeye amepata msukumo kutokana na harakati za uwindaji haramu ambao siku hadi siku umekuwa ukishika kasi.
BIBI.REHEMA amebainisha kuwa kinachomstua zaidi ni kuona kuwa kizazi kijacho kinahatari ya kujua wanyama waliopo kupitia picha kwani hatari ya uwindaji haramu ni tishio la baadhi ya wanyama kupotea kabisa katika mbuga zetu.
Matembezi hayo yanatarajiwa kupokewa Naibu Waziri wa Maliasili na utalii, BW.LAZARO NYALANDU ambayo yamepewa jina TEMBEA KWA AJILI YA TEMBO, matembezi hayo yalichokua takribani siku 19 na kutembea kilometa 650.
END.

Comments
Post a Comment