KATIBU UWT ASAIDIA WAJASIRIAMALI.
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/01-09-2013/10:59
Katibu wa
Jumuiya wa wanawake wa chama cha mapinduzi Taifa BI.AMINA MAKILAGI amekipatia
kikundi cha kinamama wajasiriamali cha WANAWAKE KWANZA, kilichopo mtaa wa Maili
Moja ka tika halmashauri ya mji wa Kibaha shilingi laki tano kwa ajili ya
kuwasaidia katika uboreshaji wa kazi zao.
Akikitembelea kiwanda kidogo cha kusindika
chakula na vinywaji baridi kinachomilikiwa na kinamama wajasiriamali wa kikundi
cha MWANAMKE KWANZA, Katibu huyo wa UWT Taifa BI.MAKILAGI amesema
wanachokifanya ni kutekeleza katiba ya jumuiya hiyo.
Na anaamini
kwa kufanya hivyo kinamama wanaweza kujikomboa kwenye matatizo ya
kisiasa,kijamii na kiuchumi kama inavyoelekeza ilani ya uchaguzi ya chama
hicho.
Naye mmoja
wa wanakikundi Mama wa Shamba wajasiriamali akisoma taarifa kwa mgeni rasmi
amesema kikundi chao cha STK MAMA KWANZA
ni kikundi cha wanawake wajasiriamali kinachoshughulika na na usindikaji
wa vyakula mbalimbali ikiwemo juice za matunda,lishe, viungo vya pilau na
viungo vya chai.
Ameongeza
kikundi hicho kimeanzishwa mwaka 2000 kikiwa na wanachama 20 walio hai, kimesajiliwa na BRELA na kina akaunti katika
Benki NMB, wamepata mafunzo ya usindikaji na ujasiriamali kutoka sehemu
mbalimbali ikiwamo Chuo Cha Kilimo Sokoine,SIDO na Chuo kikuu cha Dar es
Saalam.
END.
Comments
Post a Comment