WAKULIMA WA MBOGA WAPATIWA PAMPU
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/04-09-2013/11:09
Mbunge wa
Jimbo la uchaguzi Kibaha mjini MH. SYLVESTER KOKA akatika mfululizo wake wa
kutekeleza ahadi mbalimbali alizozitoa wakati wa kampeni ya ya uchaguzi mkuu
uliopita kwa kutoa pampu kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji katika mtaa wa
Mbwawa halmashauri ya mji wa Kibaha.
Kabla ya
kukabidhi pampu hizo kwa wananchi wa Mbwawa na Miswe MH. KOKA alitoa fursa kwa
mtendaji wa Kata ya Mbwawa, BW.TIZESA FARIS NTIRUGEREGWA ambaye amesema tatizo
kubwa linalowakabili ni maji.
BW.NTIRUGEREGWA
amefafanua kuwa wamekuwa wakikabiliwa na ukosefu mkubwa wa maji kwa takriban
miezi miwili sasa na kutokana na changamoto hiyo na nyingine kama ukosefu wa zahanati.
MH.KOKA
amebainisha kuwa kwa upande wa kero ya maji suala hilo linashughulikiwa ambapo
kwa sasa serikali imeanzisha mradi maalum wa kuhakikisha kunapatikana maji ya
kutosha kwa wananchi wanaoishi kati ya Ruvu na Kimara.
Amefafanua
kuwa ujenzi huo wa bomba kubwa la maji lenye kipenyo kikubwa ambalo litasambaza
maji kutoka katika chanzo kipya ambacho kitaanzishwa na hivyo kama mradi huo
ukikamilika utaondoa kabisa kero ya maji katika maeneo yanayokosa maji ya
uhakika.
END.
Comments
Post a Comment