WANAFUNZI WAANDAMANA KUFUATIA MGOMO WA WALIMU-KIBAHA.
Ben Komba/Pwani-Tanzania/7/31/2012/15:07
Katika hatua inayoashiria kuwa hali inayosababishwa na mgomo wa walimu unaoendelea nchi nzima athari zake sasa zimefika mbali baada ya wanafunzi wa shule za msingi za Mailimoja na Maendeleo za mjini Kibaha kuandamana wakidai haki yao ya kufundishwa kama ilivyo ada.
Wanafunzi hao ambao walikuwa wakijiongoza wenyewe huku wakipita barabara kubwa ya Morogoro wakiimba nyimbo za kudai haki ya kufndishwa na wakiitaka serikali iwalipe fedha walimu ambazo wanataka ili waweze kuendelea na masomo.
...
Mmoja ya wanafunzi ambaye nimeongea naye amesema wameamua kuandamana baada ya kuona walimu wao wanasini halafu tena wanaondoka bila kwenda madarasani kama ilivyo ada.
Kutokana na kadhia hiyo ilimbidi Diwani wa Kata ya Mailimoja kufanya kazi ya ziada akishirikiana na askari kata ili kujaribu kuwaongoza wanafunzi hao ambao walionekana kupagawa na kuchoka kutokana umbali mrefu waliotembea bila wahusika wa elimu wa kata au mji kujitokeza kuwaeleza neno lolote hao watoto wetu.
Hivi karibuni Rais wa chama cha walimu Tanzania BW. GRATIAN MKOBA alitoa taarifa kuwa mgogoro uliotangazwa na Walimu kupitia CWT, ulishindikana kusuluhishwa na msuluhishi ambaye ameteuliwa na tume ya usuluhishi na uamuzi.
Kutokana na hilo Julai 25 saa 4:30 asubuhi ndipo msuluhishi alikabidhi cheti cha kuonesha kuwa usuluhishi wa mgogoro umeshindikana, kwa kuzingatia kifungu cha 18-(1) (d) cha sheria za kazi ya ajira na mahusiano kazini ya mwaka 2004.
Ambapo taarifa hiyo ambayo imetolewa na CWT kabla ya mgomo huo, walimu wanachama wa chama hicho walipiga kura na ndipo asilimia 95 ya walimu 153.086 walipiga kura kuunga mkono mgomo huo, ambao ni walimu wa shule za awali, msingi na sekondari.
Upande wa Wazazi, BW. POLYCARP MAKUNGU ameitaka serikali kupitia watendaji wake kutoogopa kukabili maandamano yanapotokea na tena sio kwa bunduki na virungu bali kusikiliza kero zao ili ziweze kupatiwa ufumbuzi.
END.
Comments
Post a Comment