WAKAZI KIBAHA WATAKA BARABARA YAO.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/07/15/2012/09:00:39 Wakazi wa mtaa wa Mkoani Kitalu "b" katika halmashauri ya mji wa Kibaha wameshangazwa na hatua ya mhandisi wa barabara kuonyesha katika nyaraka zake kuwa baarbara ambazo zimechongwa ni kilometa 11, ili hali kazi ambayo imefanyika ni uchongaji wa kilometa 4, na kuwafanya wananchi kuhoji ni wapi kilometa 7 nyingine zilizobaki zimechongwa wapi. Diwani wa kata ya Tumbi BW. RAJAB MBENA MAKALA akizungumumza na wakazi wa eneo hilo amesema suala la kuchongewa kilometa pungufu ya mahitaji kumeleta sintofahamu kubwa kati ya wenyeviti wa mtaa katika halmshauri ya mji wa Kibaha hususan katika mtaa MKOANI BLOCK B, kutokana na halmashauri kuchonga barbara ambazo hazikuwa katika mradi ambao umeibuliwa na wananchi. Hata hivyo Diwani MAKALA ambaye amepitia tiketi ya chama cha demokrasia na maendeleo, amechukua nafasi hiyo kuwapa wananchi habari njema kuhusiana na miradi ya maendeleo ambayo imepitishwa katika kipindi cha mwaka wa fedha 2012/2013, huku barabara za lami zikiwa kipaumbele katika maeneo ya Mkoani A na Mkoani B, mradi ambao utatekelezwa kwa kushirikiana na ofisi ya mkuu wa mkoa wa Pwani. Naye Mkazi wa Mkoani Kitalu B, BI. FATMA KIARATU ameitaka halmashauri ya mji wa Kibaha kuhakikisha inafanya utaratibu wa kuwarudishia mwananchi fedha ambazo zimetozwa kinyume cha utaratibu wa ukusanyaji wa kodi za majengo, ambao umefanywa na wakala ambaye alipewa jukumu hilo JM na hatimaye kuishia kudhulumu wakazi kwa kuwabambikia madeni makubwa na baadhi kufungwa bila makosa. BI. KIARATU ameitaka halmashauri kutokuwa na upendeleo linapokuja suala la kutambua wazee ambao wanahitaji kufutiwa kodi mbalimbali kutokana na umri wao, kutoangalia wale ambao wamekuwa makazini wakato wa maisha yao bali pia uwalenge wazee wakulima ambao kila mmoja kwa wakati wake alikuwa analisaidia Taifa katika nafasi yake. END.

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA