WAKAZI WA MAILIMOJA WACHANGISHANA KUJENGA BARABARA

Ben Komba/Pwani-Tanzania/08-07-2012/10:30 Wakazi wa mtaa Muheza katika halmashauri ya mji wa Kibaha, wamekusanya jumla ya shilingi milioni 1.3, kwa ajili ya kurekebisha eneo korofi katika bonde la Mkatajika, baada ya kilio cha muda mrefu kwa halmashauri kukarabati barabara katika kata ya Mailimoja kugonga mwamba. Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Muheza BW. MOHAMED LINGOWECHE amesema wakazi wa mtaa wake wamechukua hatu hiyo kufuatia maombi yao ya kuchongewa barabar katika Kata kama kipaumbele katika kata yao kutopata majibu maridhawa, ili hali wao wakiendelea kutaabika katika msimu wa mvua. BW. LINGOWECHE amebainisha wengi wa wakazi wake ni wakulima na wafanyabiashara ndogondogo, na baada ya kuchangishana na kupatikana kiasi cha fedha, wameweza kununua mawe makubwa lori mbili,sementi mifuko 19, mchanga lori 2 na kokoto lori moja. Naye Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Tawi la Muheza, BW. AURELIUS MBENA amesema kila mwaka wao wamekuwa wakipeleka suala la kutengenezewa Barbara kama kipaumbele lakini cha kushangaza wamekuwa wakipuuzwa na maombi yao kutopewa kipaumbele, hali ambayo imewachosha wakazi wa eneo hilo kwani mpaka sasa ni takribani miaka 20 bila hatua madhubuti kuchukulia na halmashauri. BI. ANGELA MDUMA mmoja wa kinamama wanaoishi katika mtaa huo amemtaka Mbunge wa Jimbo la uchaguzi Kibaha mjini, BW. SYLVESTER KOKA kwenda kuwatembelea ili aweze kujua matatizo yanayowakabili wapiga kura wake kama alivyoahidi wakati wa kampeni kuwa kama angepata kiti hicho angetengeneza barabara kwa kutumia fedha zake mwenyewe. BIBI. MDUMA ameongeza kuwa imekuwa vigumu kwao kwenda upande wa pili ambako ndiko kuna huduma zote muhimu na hivyo kusababisha wanawake wajawazito kujifungulia majumbani na akati mwingine njiani, wanafunzi kushindwa kuhudhuria shule na wagonjwa kufia majumbani kutokana kushindwa kufikishwa hospitali katika wakati. END.

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA