VIONGOZI WA DINI WAOMBWA KUSAIDIA SENSA
Ben Komba/Pwani-Tanzania/12/07/27/8:43:24
Mkuu wa Mkoa wa Pwani BIBI. MWANTUMU MAHIZA amewataka viongozi wa dini kukemea kuporomoka kwa maadili miongoni mwa wanajamii kunakosababishwa na changamoto mbalimbali za kimaisha zinazokabili ulimwengu.
BIBI. MAHIZA amesema vitendo vya uporomokaji wa maadili vimekuwa vinaongezeka kila uchao, mpaka kufikia watu ambao wanaaminika katika jamii kujikuta nao wametubukia katika vitendo vya uvunjaji wa maadili, akitoa mfano kuwa siku hizi kusikia Padri kambaka muumini si kitu cha ajabu au mwalimu / Shekhe kabaka imekuwa kitu cha kawaida.
Amewaomba viongozi wa dini kutumia nafasi waliyonayo kuwapatia elimu waumini wao katika suala zima la kujenga jamii ambayo itakuwa inaheshimu maadili, hususan katika kupambana na vitendo vya ubakaji ambavyo vinatoa nafasi kubwa ya kuongezeka kwa maambukizi ya ugonjwa hatari wa UKIMWI.
Akizungumzia suala la Sensa Mkuu wa Mkoa wa Pwani, BIBI. MWANTUMU MAHIZA amewaomba viongozi wa dini na wazee maarufu kutumia nafasi yao katika jamii kuielimisha kuhusiana na umuhimu wa zoezi hilo, ili kuisaidia serikali katika kulikamilisha na kupatikana kwa takwimu sahihi ya idadi ya Watanzania.
Paroko wa Kanisa Katoliki la Tumbi, Padre. BEN KIKUDO amewataka Watanzania hususan wakristo kujitokeza kuhesabiwa katika kutimiza zoezi hilo maalum linalofanyika kila baada ya miaka kumi, kwa manufaa ya Taifa, na amewatoa wasiwasi makundi ambayo yamekuwa yakitilia shaka zoezi hilo wakifikiri kwamba linataka kufaidisha imani fulani.
Naye BW. MWINJUMA MATURANGA Mwenyekiti wa CUF ameelezea kusikitishwa kwake kwa kuona Waislamu wanaonewa kutokana na wenzao Wakristo kuwa wengi, kama Lutheran, Anglikan, katoliki na wengineo ilihali wao wakiwakilishwa na BAKWATA, Akahoji je ikipigwa kura wao si watashindwa,
Katika Mkutano Wakristo waliwakilishwa na Padre. BEN KIKUDO na Waislamu wakiwakilishwa na Kadhi wa Mkoa wa Pwani ALHAJI MTUPA na Shekhe wa Mkoa.
END.
hili suala la sensa nadhani serikali imechemsha kidogo. unajuwa ukiwauliza waisilamu (acha hao mashehe wa bwakwata) wanalo la msingi wanalotaka kusema. nadhani hiyo jazba yao ndo inawaponza. pia huku kwetu pia viongozi wa dini wameshindwa kutoa busara zao katika kuokoa janga hili wamebakia kushabikia dini. mimi ndivyo ninavyoona. hebu paroko wetu wakae na hao mashehe na roho wa utulivu awaingie tupate ITV live moja ili sisi tusio na dini tupate ukweli wa jambo hili la sensa. la sivyo sensa hii itakuwa ni kupoteza pesa bure huku matatizo lukuki k.m hospitali, madaktari migomo, walimu migomo, mgao wa umeme vikituandama.
ReplyDelete