MWEKEZAJI ASAIDIA KIJIJI/ JENGO LA PCCB PWANI LAZINDULIWA

Ben Komba/Pwani/Tanzania/7/6/2012 9:31:29 AM Wakazi wa kijiji cha Lukenge Kata ya Magindu wamewezeshwa kupata maji safi ya kunywa , josho na bwawa la kufuga samaki ambalo halitakauka katika kipindi chote cha mwaka. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Kaimu Mkurugenzi wa kampuni ya TWO BROTHERS INVESTMENT, inayomilikiwa na wawekezaji wa ndani, BW. YUSUPH MJEMA amesema kampuni yao inajihusisha na kilimo mseto, ufugaji wa samaki, kunenepesha ng,ombe na kilimo kwanza. BW. MJEMA amebainisha kuwa huduma hizo zinatarajiwa kuzinduliwa rasmi na mkuu wa mkoa wa Pwani, BIBI. MWANTUMU MAHIZA siku ya Jumanne Julai 10 mwaka huu katika shamba hilo lenye eka 400. Amefafanua kati ya eka hizo 400, bwawa pekee lina urefu na urefu wa mita 186 na kina cha futi 40, na mpaka sasa wameshaotesha mbegu za samaki 500 ambazo wamezinunua kutoka SUA za samaki aina ya Sato. BW. MJEMA ameongeza kuhusiana na suala la kilimo kwanza mpaka sasa wamelima mahindi ambayo yanatarajiwa kuvunwa wakati wowote katika ekari 300 za shamba hilo, Mbali ya hayo kampuni ya TWO BROTHERS INVESTMENT imesaidia kuajiri vijana 8 kutoka kijijini hapo na kupatiwa mafunzo kutoka katika Chuo kishiriki cha kilimo Sokoine, ikiwa pamoja na kujenga madarasa mawili ya shule ya msingi, kujenga ofisi ya kijiji na kukarabati zahanati. Aidha BW. MJEMA amezungumzia suala la changamoto zinazowakabili ni wasafirishaji wa mifugo kuingiza ng’ombe nyakati za usiku na kuharibu miundo mbinu ya shamba hilo mseto. END. JENGO LA PCCB PWANI LAZINDULIWA Mkurugenzi wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa Tanzania, BW. EDWARD HOSEAH amewataka wahusika wa masuala ya kodi kuangalia upya viwango viwango vya kodi vinavyopangwa ili kupunguza ushawishi wa utoaji na upokeaji rushwa nchini. BW. HOSEAH amesema hayo wakati wa uzinduzi wa Jengo la taasisi hiyo mjini Kibaha, ambapo amebainisha kuwa uwepo wa kodi nyingi kwa wafanyabiashara imekuwa kichocheo kikubwa cha rushwa hasa kutokana na kodi hizo kumuumiza mfanyabiashara na kuamua kutumia rushwa ili kujipatia nafuu. Akizungumzia juu ya jengo hilo amesifu ushirikiano ulioonyeshwa na taasisi nyingine kuwezesha ujenzi wa jengo hilo ambalo limegharimu takribani shilingi bilioni moja za kitanzania, na ameaahidi PCCB Taifa kutoa samani na fedha za kuliendesha jengo hilo ambalo ni moja kati ya majengo 8 yaliyojengwa na PCCB, kati ya hayo manne ni ofisi za wilaya. Akimwakilisha mkuu wa mkoa wa Pwani, Katibu tawala wa mkoa, BI. BERTHA SWAI amewataka watumishi wa taasisi hiyo kufanya kazi kwa kufuata misingi ya haki na uadilifu bila kumuone au kumpendelea mtu yoyote ili kufikia malengo ya uwepo wa taasisi hiyo. Aidha ameipongeza taasisi hiyo kwa kufanikiwa kuwakamata baadhi ya watuhumiwa wa makosa ya rushwa na kuwafikisha mahakamani, hatua mabayo inaleta matumaini kwa jamii. END.

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA