MAANDALIZI YA SENSA YAPAMBA MOTO PWANI.
Ben Komba/Pwani-Tanzania/17-Jul-12 9:46 AM
Mafunzo ya sensa ngazi ya pili kwa ajili ya kuwaandaa makarani na wasimamizi ambao wamelengwa kwenda kulisimamia zoezi hilo katika maeneo watakayopangiwa.
Kiongozi wa timu ya wakufunzi wa sensa Mkoa wa Pwani, DOKTA. SIMON MSANJILA ambaye pia ni mkuu wa kitivo cha Sayansi na Teknolojia, chuo kikuu cha Mzumbe amesema mafunzo hayo ni zoezi ambalo limelenga kuboresha ukusanyaji wa takwimu.
DOKTA. SIMON amefafanua kundi hilo ambalo linapatiwa mafunzo ni kutoka katika idara mbalimbali ikiwa elimu, mipango na uwakilishi wa makundi maalum likiwemo la walemavu.
Akizungumzia changamoto zinazokabili maandalizi ya zoezi la sensa katika mkoa wa Pwani, BW. MSANJILA amesema ni kuchelewa kwa vifaa muhimu kwa ajili ya zoezi hilo, kuchelewa kwa uwezeshaji kwa washiriki wa mafunzo, ambavyo baadhi wameweza kuzishinda.
Amesisitiza kuwa zoezi la kuhesabu limegawanyika katika makundi manne ambayo ni kaya za kawaida ambao watakutwa nyumbani, kaya maalum yaani kwa watakaokuwepo mahospitalini, Polisi, magereza na kwenye nyumba za wageni.
Mratibu wa sensa mkoa wa Pwani, BW.PHILEMON MWENDA amesema timu ya sensa Mkoa wa Pwani wamejipanga vyema kuhakikisha zoezi hilo linafanikiwa na wasimamizi na makarani 3800 wameshapangiwa vituo tayari kwa kukusanya takwimu za sensa ya watu na makazi.
END.
Ben Komba/Pwani-Tanzania/17-Jul-12 10:02:50 AM
Shirika lisilo la kiserikali la VOLUNTEERS FOR SOCIAL CHANGE-VSC- la wilayani Kisarawe limeanzisha programu maalum ya kuwawezesha wanawake, vijana na watoto wanaoishi katika mazingira magumu kujikimu kwa kutumia mbinu za kijasiriamali.
Mwandishi wa habari hizi akiongea na Mwezeshaji jamii wa shirika hilo, BI. STELLA PHILEMON ofisini kwake, amesema lengo lao kubwa ni kutoa mafunzo ya ujasiriamali kwa makundi maalum ambayo kwayo wakipatiwa mafunzo hayo kutawawezesha kujipatia kipato.
BI. PHILEMON ameongeza toka kuanza kwa programu hiyo tayari wameshatoa mafunzo katika awamu mbili, ambapo washiriki wamepatiwa utaalamu wa kutengeneza sabini za maji na ngumu, sabuni za dawa za kuogea na jam ya mkate.
BI. PHILEMON amebainisha kuwa wamekuwa wakikutana na vikwazo mbalimbali ikiwa pamoja na wajasiriamali kutokuwa tayari kutoa fedha kwa ajili ya kununulia malighafi za mafunzo na wengi wao kutojali muda wa kuhudhuria mafunzo katika kipindi mwafaka.
END.
Comments
Post a Comment