MAONI KATIBA KATA YA MAILIMOJA.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/2012-07-22/1:54:32 PM Shirika lisilo la kiserikali la Pwani-DPA kwa kushirikiana na ofisi ya serikali ya Mailimoja wametoa mafunzo ya awali kwa wakazi wa mtaa huo tayari kukutana na tume ya kukusanya maoni juu ya uandikaji wa katiba mpya ili kutoa fursa yakuwepo na ufahamu juu ya katiba angalau kidogo kwa wakazi hao. Mwezeshaji katika mazungumzo hayo yanayohusiana na utoaji wa elimu ya uraia kwa jamii katika kuwajengea uwezo wananchi wa kujadili kuhusiana na uandikaji wa katiba mpya, kutoka shirika lisilo la kiserikali la YOUTH PARTNERSHIP COUNTRYWIDE, BW. MARTIN MUNG'ONGO amesema kuwa mageuzi ya kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni ni jambo ambalo haliepukiki toka wakati ndio unaozungumza na hivyo wananchi hawana budi kutumia fursa hii adimu kuamua mambo yatakayokuwa na manufaa kwa kizazi kijacho. Ameongeza kwa jamii kukubali kufanya mabadiliko ambayo yananuia kuleta mabadiliko ya kiuchumi, kisiasa na kitamaduni ndipo hapo nchi inapopiga hatua kuelekea kwenye maendeleo, ili mradi mageuzi hayo yasilenge katika kukweza makundi fulani katika jamii kutokana na Kabila, dini au Rangi, amesisitiza kuwa jukumu la kubadili mfumo wowote nchini upo mikononi mwa binadamu na iwapo binadamu asipochukua hatua ya kufanya mageuzi kwa lengo la kuboresha basi maendeleo Duniani yatasimama. BW. MUNG'ONG'O amebainisha badala ya watu kwenda kutoa maoni kwa jazba na wengine wakitumia imani kwa kuziweka mbele na kusahau utaifa, sera ambazo haziwezekani kwa vile tu labda Uganda wamefanya hivyo, na kuwakumbusha wananchi Uganda wanautamaduni wa kufanya mambo yao na sisi tuna wa kwetu ambao umelenga kuheshimu imani ya kila Mtanzania bila serikali kulazimika kupendelea upande fulani wa dini, mfano mwingine ambao ametoa ni Kenya ambapo Bunge lao kupigana sio kitu kigeni, lakini Watanzania siku tumekuwa wa kutatua matatizo yetu kwa kuongea. Akiongea katika mkutano huo wa mtaa, Mkurugenzi mtendaji wa Pwani-DPA, BW. MATTHEW CHUNGU ameeleza lengo la shirika lake kutoa elimu hiyo ya uraia ni kujaribu kuwapatia mwanga wa kujua Katiba ya zamani kabla ya kukutana na tume ya ukusanyaji wa maoni juu ya uandikaji katiba mpya utakaofanyika katika kiwanja cha mpira Maili moja saa tatu asubuhi, Julai 23. na hilo linatokana na wananchi wengi kutojua katiba ipasavyo kiasi kwamba wengi wao kufuata mkumbo kuongelea mambo ambayo yanaweza kuhatarisha amani iliyopo nchini kwa sasa kama tunavyoshudia. Mkazi wa mtaa wa Mailimoja BIBI. PETRONELA KISALALA ameitaka serikali kutojihusisha na masuala ya dini na kuendelea kuwa kama ilivyo sasa ikiwa pamoja na kutokubali kujiunga na OIC na kuanzishwa mahakama ya Kadhi kuingizwa katika Katiba, na kutaka wahusika wanaotaka hivyo kupitia dini zao kujiunga na taasisi hizo na wafaidike na mema yatokanayo kwayo. END.

Comments

  1. mahakama kuu iruhusu watu kuabudu dini zao bila kuingiliwa; hivyo nashauri mahakama za Tz zisiingilie maamuzi ya mahakama ya kadhi pindi taasisi za dini zitakapoanzisha mahakama hizo. na katiba ya Tz iheshimu uhuru wa kuabudu na iainishe dini zinazotambulika hapa nchini.isiwe holela tu kama inavyotokea huko zambia na mikoa ya kusini Tz ambako kuna utitiri wa makanisa na dini mbalimbali.

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA