MATREKTA YAPUNGUA BEI, KILIMO JUU?
Ben Komba/Pwani-Tanzania/13-Jul-12/18:33:10
Mkuu wa wilaya ya Kibaha BIBI. HALIMA KIHEMBA amewataka wawekezaji katika kilimo kutumia fursa ambayo imetolewa na serikali ya kupunguza bei ya matrekta katika kuwawezesha wakulima kuzalisha chakula kwa wingi katika harakati za suala zima la kukuza uchumi unaotegemea kilimo katika sehemu kubwa toka kuna ardhi yenye rutuba ya kutosha.
BIBI. KIHEMBA ameongea hayo akizindua shamba la kilimo mseto katika kijiji cha Lukenge kwenye kata ya Magindu wilayani Kibaha mkoa wa Pwani, ambalo linamilikiwa na mwekezaji wa ndani ambaye ni mfugaji BW. TANGONO MAHOMBELO KASHIMBA kupitia kampuni yake ya uwekezaji ya TWO BROTHERS INVESTMENT, ambapo amesema amefurahishwa na jinsi mwekezaji huyo alivyoweza kujenga miundombinu katika eneo lake hilo, ikiwa pamoja na kuchimba bwawa la maji ambalo kwa sasa limekuwa tegemeo kwa jamii ya hapo.
BIBI. KIHEMBA ameongeza kwa kuwekeza katika kilimo mseto imewezesha uwepo wa matumizi bora ya ardhi mpango ambao umeasisiwa na serikali katika kuhakikisha vijiji vinapangwa kwa kuzingtia masuala muhimu ya mkilimo na ufugaji katika kuepusha migogoro isiyo na lazima katika jamii.
Akizungumzia hatua ambazo serikali imezichukua mpaka sasa kwa lengo la kukipa mafanikio kilimo mseto ni pamoja na kuajiri afisa samaki ambaye atakuwa na wajibu wa kutoa ushauri wa kitaalamu kwa wafugaji wa samaki kama ilivyo kwa wawekezaji hao TWO BROTHERS INVESTMENT, na amewashauri wawekezaji hao kuwekeza katika ufugaji wa nyuki toka wana eneo la kutosha kwa shughuli hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo BW. TANGONO KASHIMBA ameiomba serikali kuwaunga mkono wakulima wa kilimo mseto kama ambavyo imefanya kwa kuunguza bei matrekta na pembejeo nyingine ili kukipa nguvu kilimo kwanza kwani kwa kuwakopesha wakulima au kuwauzia bei nafuu kutaweza kuleta mapinduzi ya kilimo.
BW. TANGONO amefafanua kuwa maarifa ya kuanzisha uwekezaji katika kilimo mseto ameupata baada ya kupatiwa mafunzo katika chuo cha LITI, Morogoro ambapo yeye akiwa mmoja wa wafugaji wakubwa walipatiwa mbinu ya kufuga ng'ombe kisasa kwa kuchanganya na shughuli zingine badala ya kutegemea ng'ombe pekee.
Aidha kutokana na elimu hiyo imemuwezesha kujenga josho kwa ajili ya ng'ombe wake na majirani wanaomzunguka, kujenga Bwawa la samaki, kujishughulisha na kilimo cha mahindi na kuanzisha shamba la majani sawa na kutunza mazingira katika eneo linalomzunguka ambalo limejitenga mbali kabisa na kjiji cha wenyeji wengine.
END
--- On Sun, 13/7/12, Bernard Komba wrote:
WAJITOLEA KUIMARISHA MIUNDOMBINU
Ben Komba/Pwani-Tanzania/13-07-2012/10:30
Wakazi wa mtaa Muheza katika halmashauri ya mji wa Kibaha, wamekusanya jumla ya shilingi milioni 1.3, kwa ajili ya kurekebisha eneo korofi katika bonde la Mkatajika, baada ya kilio cha muda mrefu kwa halmashauri kukarabati barabara katika kata ya Mailimoja kugonga mwamba.
Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Muheza BW. MOHAMED LINGOWECHE amesema wakazi wa mtaa wake wamechukua hatu hiyo kufuatia maombi yao ya kuchongewa barabar katika Kata kama kipaumbele katika kata yao kutopata majibu maridhawa, ili hali wao wakiendelea kutaabika katika msimu wa mvua.
BW. LINGOWECHE amebainisha wengi wa wakazi wake ni wakulima na wafanyabiashara ndogondogo, na baada ya kuchangishana na kupatikana kiasi cha fedha, wameweza kununua mawe makubwa lori mbili,sementi mifuko 19, mchanga lori 2 na kokoto lori moja.
Naye Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Tawi la Muheza, BW. AURELIUS MBENA amesema kila mwaka wao wamekuwa wakipeleka suala la kutengenezewa Barbara kama kipaumbele lakini cha kushangaza wamekuwa wakipuuzwa na maombi yao kutopewa kipaumbele, hali ambayo imewachosha wakazi wa eneo hilo kwani mpaka sasa ni takribani miaka 20 bila hatua madhubuti kuchukulia na halmashauri.
BI. ANGELA MDUMA mmoja wa kinamama wanaoishi katika mtaa huo amemtaka Mbunge wa Jimbo la uchaguzi Kibaha mjini, BW. SYLVESTER KOKA kwenda kuwatembelea ili aweze kujua matatizo yanayowakabili wapiga kura wake kama alivyoahidi wakati wa kampeni kuwa kama angepata kiti hicho angetengeneza barabara kwa kutumia fedha zake mwenyewe.
BIBI. MDUMA ameongeza kuwa imekuwa vigumu kwao kwenda upande wa pili ambako ndiko kuna huduma zote muhimu na hivyo kusababisha wanawake wajawazito kujifungulia majumbani na akati mwingine njiani, wanafunzi kushindwa kuhudhuria shule na wagonjwa kufia majumbani kutokana kushindwa kufikishwa hospitali katika wakati.
END.
Comments
Post a Comment