MWENYEKITI WA CCM WILAYA YA KISIASA KIBAHA MJINI MATATANI
Ben Komba/Pwani-Tanzania/3/17/2012 1:36:44 PM
Katika kile kinachoashiria kuongezeka kwa migogoro ya ardhi kulikosababishwa na viongozi wa serikali za mitaa na vijiji waliomaliza muda wao kuuza maeneo bila kufuata taratibu za kisheria, Imelililazimu Baraza la ardhi la kata ya Tumbi kuhamia mtaa wa Boko Temboni ambalo limezua mgogoro kwa pande mbili ambazo kila moja inadai ni eneo lake.
Katika tukio moja la aina hiyo hatimaye lilimfikisha katika Baraza la ardhi kata ya Tumbi, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi mjini Kibaha, BW. MAULID BUNDALA, kujibu tuhuma ya kuhusika kwake katika kuuzwa kwa shamba la Marehemu, BW. JOHN BAYONA, Kwa mtu mwingine BW. SEGE MWAKISALE, Wakati huo yeye akiwa mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Boko Temboni.
Mlalamikaji katika shauri hilo, BI. ASTRIDE BAYONA ameliambia baraza la ardhi la kata ya Tumbi kuwa eneo ambalo BW. MWAKISALE ameuziwa ni mali ya marehemu Baba yake, na mtu aliyeuza eneo hilo BW. ABDALLAH ONYANGO alikuwa ni mwangalizi aliyewekwa kulitunza shamba hilo.
BI. BAYONA amebainisha kuwa Marehemu Mzee wao alinunua shamba hilo kutoka kwa PROFESA PHILIP BATHONDI, na kumuweka BW. ONYANGO kama msimamizi, lakini cha kushangaza BW. ONYANGO alipokuwa anauza shamba hilo alipata baraka zote toka serikali ya mtaa wa kipindi hicho kuwa hilo eneo ni mali yake bila vithibitisho vyovyote, Kwa kile ambacho mashahidi akiwemo Mwenyekiti huyo wa CCM mjini Kibaha, BW. BUNDALA MAULID BUNDALA kuwa kwa sababu walikuwa wakimuona analima eneo hilo basi wakajiridhisha kuwa ni lake.
BI. BAYONA alimuuliza swali Mwenyekiti huyo wa CCM, BW. BUNDALA kuwa ukimuona mtu analima sehemu fulani mara kwa mara je hiyo inamhalalishia yule mtu umiliki wa eneo fulani?
Ambapo mwenyekiti huyo wa chama cha mapinduzi mjini Kibaha alijibu kuwa yeye akiwa mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Boko Temboni alimtambua BW. ONYANGO kama ndio mmiliki halali wa eneo hilo na sio Marehemu JOHN BAYONA, Hivyo hakuona umuhimu wa BW. ONYANGO kuleta uthibitisho kama eneo analouza ni lake kweli.
Baraza hilo la kata ya Tumbi lililofika katika eneo la tukio liliambatana na Katibu wake JOHN MZUGUNO, Mwenyekiti BIBI. ANGELINA KISUNGA na wajumbe araza hilo, BW. OMARI KIBUMBANO, BW. ALI MBEMBENI na BI. MARY WILLIAM, ambapo hukumu juu ya shauri hilo itatolewa April 24 mwaka huu katika ofisi ya kata ya Tumbi.
Hivi sasa serikali imeamua kuyafanyia kazi migogoro ya ardhi na kufananisha ukiukwaji wowote wa taratibu za ardhi unatishia uvinjifu wa amani katika jamii.
END

Comments
Post a Comment