MAADHIMISHO YA WIKI YA MAJI YAANZA MJINI KIBAHA
Ben Komba/Pwani-Tanzania/3/17/2012Friday, March 16, 2012/08:25:17 PM
Halmashauri ya wilaya ya Kibaha, inatarajia kuwa na mamlaka yake yenyewe ya maji iwapo itafanikiwa kupata chanzo tofauti na Mto Ruvu, kutokana na mto huo kushindwa kukidhi mahitaji kwa watumiaji wa maji kutokana na kuzidiwa uwezo.
Mhandisi wa maji wilayani Kibaha, MHANDISI. CHRISTOPHER MDUMA ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa wiki ya maji ambayo umefanyika Mlandizi, ambapo amesema kuna masharti ya kuwa na mamlaka ya maji, na mojawapo ni kuwa na chanzo kipya cha uhakika ambacho kitaweza kusambaza maji katika vijiji mbalimbali.
Mhandisi MDUMA amebainisha kwa sasa, wilaya za mkoa wa Pwani za Bagamoyo, Kisarawe na Kibaha zipo chini ya DAWASA, na hii ni kutokana na Mkoa wa Dar es Saalam kuegemea chanzo kwa wakazi wake kiasi cha kushindwa kutosheleza mahitaji ya wakazi wa Jiji.
Akifafanua kuhusu uwezekano wa Kibaha kuwa na mamlaka yake yenyewe ya maji upo, na kinachofanyika ni kufuatilia kwa karibu chanzo cha maji kilichopo katika kijiji cha Ngeta ambacho kinatoa wastani wa lita 36,000 kwa sasa, na hivyo kuleta matumaini makubwa ya miaka ya karibuni kuweza kuwa na mamlaka yake yenyewe.
Naye mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kibaha, MH. MANSOUR KISABENGO amewataka watendaji wa kata zote kuwasisitizia wananchi juu ya umuhimu wa kutunza vyanzo vya maji, ingawa sio kila mwananchi anajua umuhimu wa utunzaji wa vyanzo vya maji lakijni anaamini kama wakipatiwa elimu ya kutosha kuna uwezekano mkubwa wa kutokea mabadiliko katika sekta ya maji.
MH. KISABENGO amekemea tabia ya baadhi ya wananchi kulima ukingoni mwa chanzo vyanzo vya maji, kwani kwa kufanya wanasababisha uharibifu katika vyanzo na kuisababishia jamii dhiki kutokana na kukosekana kwa maji safi na salama.
Aidha ameiomba serikali kuharakisha mradi wa maji wa WAMI-CHALINZE ambao uteekelezaji wake unasuasua kutokana na sababu ambazo hazipo bayana, na hivyo kuvifanya vijiji vya Magindu, Lukenge naGwata kuendelea kudhikika kila inapofika wakati wa kiangazi.
END.

Comments
Post a Comment