Ben Komba/Pwani-Tanzania/3/23/2012 5:19:44 PM
Halmashauri ya wilaya ya Kibaha kwa mara ya kwanza imezindua Baraza lake la wafanyakazi lenye jukumu la kuwashirikisha wafanyakazi wa halmashauri katika utekelezaji wa shughuli za halmashauri kwa kushirikiana na uongozi.
Akizungumza katika uzinduzi wa baraza hilo katibu tawala wilaya ya Kibaha, BW. JUSSEIM MWAKIPESILE akimwakilisha mkuu wa wilaya HAJAT HALIMA KIHEMBA, amesema baraza hili ni mwanzo mpya wa kihistoria kwa halmashauri ya wilaya ya Kibaha ikiwa kama sehemu ya sera ya kushirikisha wafanyakazi katika kila Nyanja ya halmashauri.
Na lengo kubwa likiwa ni kuongeza ufanisi mahali pa kazi ikiwa pamoja na kuboreha utendaji wa utumishi wa umma kwa kutoa huduma stahili kwa mteja anapohitaji kwa kuzingatia maadili na sheria za kazi zinazomzunguka mfanyakazi.
Aidha BW. MWAKIPESILE amebainisha kuwa baraza la wafanyakazi lina wajumbe wa kuteuliwa, wajumbe wa kuchaguliwa na wajumbe ambao wanaingia barazani kwa nyadhifa zao, hivyo amesisitiza umoja na mshikamano kama nguzo pekee ya kuiwezesha halmashauri kutimiza malengo iliyojiwekea.
Naye Afisa elimu kazi kutoka tume usluhishi na uamuzi –CMA- , BI. MODESTA NGOLI amesema baraza la wafanyakazi ni chombo ambacho kinatoa fursa kwa wafanyakazi kushirikishwa kikamilifu katika maamuzi mbalimbali yanayofanyika mahali pa kazi ambayo kwa njia mojq au nyingine yanaweza kugusa maslahi yake kama mfanyakazi.
BI. NGOLI ameongeza mabaraza ya wafanyakazi yalianza kuundwa kufuatia mapinduzi ya viwanda yaliyofanyika katika nchi za Magharibi ambapo waajiri kwa ajili ya kujipenda waliwanyonya wafanyakazi kiasi cha kuanzisha migomo ambayo baadaye iliuleta majadilano na kuanza kuonekana umuhimu wa kuwepo kwa mabaraza ya wafanyakazi, ili kero zote sehemu za kazi zifikishwe hapo mkwa ajili ya kufanyiwa kazi.
END.
MAFUNZO YA UREFA
Ben Komba/Pwani-Tanzania/23-07-2013/10:03 Chama cha marefa wilayani Kibaha kinaendesha program maalum ya mafunzo kwa marefa wapya wenye kutaka kujiendeleza kuwa waamuzi katika ngazi mbalimbali za ligi za mchezo huo. Katibu wa Chama cha marefa wilayani Kibaha ambaye pia ndio refa bora wa ligi ya VODACOM msimu uliopita BW.SIMON MBELWA amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwezesha kuzalisha marefa wapya. BW.MBELWA amefafanua kuwa katika mambo ambayo yatazingatiwa katika mafunzo hayo ni ufundishaji wa sheria 17 za soka ambazo kila mwamuzi anapaswa kuzifahamu kwa ufasaha ili kuepusha malalamiko na wakati mwingine hata vurugu katika mchezo huo. Naye mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo, BW. GEORGE amesema kwa kupatiwa mafunzo hayo kutawasaidia kufanya maamuzi yaliyo sahihi wakati wakichezesha mechi za michuano mbalimbali. END.
Comments
Post a Comment