BEN KOMBA/PWANI-TANZANIA/3/22/2012 8:35:45 PM Suala la maji safi na mazingira ni miongoni mwa maeneo ambayo yamo katika nguzo kuu katika kuboresha maisha na ustawi wa jamii katika utekelezaji wa MKUKUTA. Katibu tawala wilaya ya Kibaha BW. JUSSEIM MWAKIPESILE ameyasema hayo wakati wa maadhimisho ya wiki ya maji ambayo kiwilaya yamefanyika katika mji mdogo wa Mlandizi. Ambapo BW. MWAKIPESILE amesema serikali katika kuhakikisha inakabiliana na uhaba wa maji na kuboresha usafi wa mazingira kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo imeanzisha program ya maji na usafi wa mazingira kwenye vijiji ambavyo vinakabiliwa na uhaba wa mkubwa wa maji. Amefafanua kuwa program hiyo imeanza toka mwaka 2006 na inatarajiwa kukamilika mwaka 2025 na lengo kuu ni kuhakikisha wananchi wote wanapata maji safi na salama karibu na makazi yao ifikapo mwaka 2025 sambamba na dira ya maendeleo. Awali mhandisi wa maji katika halmashauriWilayani Kibaha, BW. CHRISTOPHER MDUMA amebainisha kuwa maadhimisho ya wiki ya maji wilyanai Kibaha yameadhimishwa kwa kufanya shughuli mbalimbali, ikiwemo warsha kwa wadau wa maji kwa kujadili na kuweka mikakati kuhusiana na utunzwaji wa vyanzo vya maji, uanziushwaji wa sera wa jumuiya za watumiaji maji, Ikiwa pamoja na kupitia sera ya maji na sheria ya maji na pia kamati ya maji na usafi wa mazingira imefanya mikutano ya awali na serikali za vijiji na kamati za maji za vijiji vya Kitomondo, Minazi Mikinda,, Ruvu Stesheni na Soga katika kipindi cha maadhimisho ya weiki ya maji Kauli Mbiu ya maadhimiosho ya wiki ya maji ni”MAJI KWA USALAMA WA CHAKULA”. END.

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA