Ben Komba/Pwani-Tanzania/3/24/2012 5:05:02 PM
Chama cha waandishi wa habari wa mazingira na za watu wenye ulemavu Mkoani Pwani, (PEDWA) wamekutana leo kwa mara ya kwanza katika kupanga mkakati wa kuanza baadhi ya shughuli zake kwa kutumia nguvu zake yenyewe ili kuonyesha umuhimu wa masuala ya mazingira na ya watu wenye ulemavu katika jamii.
Katika kikao cha pamoja na baadhi ya wadau wa masuala hayo, Mwenyekiti wa PEDWA- PWANI ENVIROMENTAL AND DISABLED WRITERS ASSOCIATION, BW. BERNARD KOMBA amesema lengo la kuanzishwa kwa asasi hiyo isiyo tengeneza faida, ni kuielimisha jamii juu ya umuhimu wa utunzaji wa mazingira na kuthamini watu wenye ulemavu.
BW. KOMBA amebainisha kuwa jamii bado inafanya dhihaka juu ya masuala hayo ambayo kuyatekeleza ni sawa na kutekeleza hqaki za msingi za binadamu, hasa ikizingatiwa binadamu wana haki ya kuishi katika mazingira yatakayomwezesha kufanya shughuli zake bila kusumbuliwa na majanga ya asili yanayosababishwa na ukataji misitu holela.
Aidha kwa upande wa walemavu kutekeleza haki zao ni kutekeleza haki za msingi za binadamu kwani nao wanastahili kuthaminiwa na kupatiwa huduma wanazostahili katika kuboresha maisha yao ya kila siku, hivyo ni juu ya serikali na jamii kuhakikisha watu wenye ulemavu wanapatiwa haki zao.
Mmoja wa wadau ambaye amehudhurio kikao hicho cha utambulisho kutoka kampuni ya mafuta ya KOBIL ya Chalinze wilayani Bagamoyo, BW. RAJAB VARISANGA akizungumzia juu ya suala la mazingira, amewashauri watanzania wabadilike na kuanza kutumia gesi hasa kutokana nishati hiyo kuwa nafuu kulinganisha na mkaa, mtumiaji akielimishwa juu matumizi sahihi ya gesi.
BW. VARISANGA amebainisha katika utafiti alioufanya amegundua ukiwa na mtungi wa gesi wa shilingi elfu 28, unaweza kutumia kwa kipindi cha miezi mitatu, ambapo katika kipindi hicho kuna uwezekano mkubwa wa kutumia gunia 6 zenye thamani ya shilingi elfu 90, ambapo ametaka chama hicho kusaidia kutoa elimu hiyo kwa wananchi ili kuwezeshja kupunguza matumizi ya mkaa, na hasa ikizingatiwa nchi yetu ina gesi lukuki.
Naye Mdau mwingine BW. MAGID YAHYA OMARY kutoka kampuni ya mafuta ya KOBIL nayo inayotoa huduma zake maeneo ya Chalinze, ameitaka serikali kuzuia ukataji wa miti na wananchi ikiwezekana walazimishwe kupanda miti ili kuiokoa nchi isikumbwe na jangwa linalotunyemelea kwa kasi.
END
MAFUNZO YA UREFA
Ben Komba/Pwani-Tanzania/23-07-2013/10:03 Chama cha marefa wilayani Kibaha kinaendesha program maalum ya mafunzo kwa marefa wapya wenye kutaka kujiendeleza kuwa waamuzi katika ngazi mbalimbali za ligi za mchezo huo. Katibu wa Chama cha marefa wilayani Kibaha ambaye pia ndio refa bora wa ligi ya VODACOM msimu uliopita BW.SIMON MBELWA amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwezesha kuzalisha marefa wapya. BW.MBELWA amefafanua kuwa katika mambo ambayo yatazingatiwa katika mafunzo hayo ni ufundishaji wa sheria 17 za soka ambazo kila mwamuzi anapaswa kuzifahamu kwa ufasaha ili kuepusha malalamiko na wakati mwingine hata vurugu katika mchezo huo. Naye mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo, BW. GEORGE amesema kwa kupatiwa mafunzo hayo kutawasaidia kufanya maamuzi yaliyo sahihi wakati wakichezesha mechi za michuano mbalimbali. END.
Comments
Post a Comment