ABAKA MTOTO WA MIAKA 3

Ben Komba/Pwani-Tanzania/3/27/2012 6:41:51 PM Mtoto mdogo anayesoma shule ya chekechea mwenye umri wa miaka mitatu na miezi minane amebakwa leo jioni hii na kijana aliyejulikana kwa jina moja la JUSTIN mwenye umri wa miaka 20 na kusababishiwa maumivu makali katika maeneo ya Mpakani mjini Kibaha. Kwa mujibu wa mzazi wa mtoto BIBI. ASHURA WAZIRI amesema kama kawaida mtoto wake alirudi shule , na akambadilisha nguo na akaenda kucheza na mwenzake, wakati akicheza huku kijana yule mbaya JUSTIN alikuwa anafua nguo zake uwani katika nyumba hiyo ya kupanga. JUSTIN ambaye anafanya kibarua cha kuchoma kuku eneo la Maili Moja majira ya jioni, inasemekana hana hata miezi miwili toka alipowasili kutoka Mkoani Iringa, mtoto huyo kama mtoto mwingine yoyote alikuwa na upendo na wapangaji wengine wote hivyo kuingia chumba kimoja hadi kingine kwake ilikuwa kawaida. Lakini tofauti na siku nyingine mtoto huyo aliingia chumbani alichokuwa analala JUSTIN huku Mama yake akiwa dukani ambako amejiajiri hakujua mtoto huyo kama ameingia chumbani mle. Ndipo mtoto huyo alikwenda kwa mama yake huku amenyanyua gauni akimwambia Mama yake kuwa Mama JUSTIN ameniumiza huku na Mama yake alipomkagua vizuri alimkuta amechafuka akiwa ametapakaa mbegu za kiume na akimgusa alikuwa akilia kwa uchungu akisema anaumia. Kutokana na hali hiyo wapangaji wote kwa wakakaa kujua ukweli wa jambo hilo, lakini wakati wote kijana JUSTIN alikuwa kimya bila kujibu chochote, mpaka hatimaye baada ya kubanwa sana amesema kuwa alichokifanya yeye ni kumchezea na vidole vyake lakini cha kushangaza ni wapi mbegu za kiume zilizoonekana zimetoka. Hatimaye Wazazi wa mtoto walichukua hatua ya kwenda kutoa taarifa kituo kidogo cha Polisi Maili Moja kwa ajili ya kuchukuliwa hatua za kisheria dhidi ya mtuhumiwa, mpaka naondoka eneo hilo majira ya sa kumi na mbili jioni Baba wa mtoto huyo na motto walikuwa bado hospitali katika kutafuta uthibitisho ambao utatumika kama kielelezo kesi itakapoanza kusomwa. END.

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA