SHERIA YA HUDUMA ZA MAJI NA USAFI WA MAZINGIRA YA MWAKA 2009

Ben Komba/Pwani-Tanzania/3/18/2012 8:01:57 PM

Halmashauri ya wilaya ya Kibaha imeazimia kuanza kutekeleza kwa vitend sheria ya huduma za maji na usafi wa mazingira ya mwaka 2009, sheria ambayo imetungwa kwa dhumuni la kuweka masharti ya usimamizi na uendeshaji wa huduma za maji na usafi wa mazingira.

Akizungumza katika maadhimisho ya maji yanayoendelea mpaka yatakapofika kilele hapo MARCH 03, Mwanasheria wa halmashauri ya wilaya ya Kibaha, BI.SALAMA MANGARA amesema sheria hiyo imefafanua juu ya wajibu wa wadau mbalimbali katika uendeshaji wa miradi ya maji katika ngazi ya jamii.

BI. MANGARA amefafanua kuwa pamoja na mambo mengine sheria inazungumzia uanzishwaji wa vyombo vya kisheria vya watumiaji maji yaani “community owned water supply organisation (COWSO).

Amebainisha kuwa serikali itakuwa na jukumu nla kufanya mapitio ya sera ya maji pale itakapohitajika, kutoa mwongozo wa jinsi ya kuunda kusajili, kusimamia, na kuongoza vyombo vya watumiaji maji kwa ushirikiano na halnmashauri za wilaya, miji, manispaa na maji

katika ngazi ya halmashauri BI. MANGARA ameweka wazi ni pamoja na kuteua msajili wa vyombo vya watumiaji maji vitakavyofanya kazi chini ya sheria ya huduma za maji na usafi wa mazingira ya mwaka 2009 sawa na kutoa fidia kwa wote watakaoharibiwa mali zao wakati wa upanuzi wa shughuli za maji.

Ambapo halmashauri itasaidia kupatikana kwa ruzuku kwa ajili ya gharama zinazodaiwa na serikali na taasisi zake, kwa mfano: umeme, madawa na itakuwa na wajibu wa kuteua afisa watakaoratibu shughuli za uendeshaji na matengezo ya miradi ya maji mna usafi wa mazingira, katika vijiji vyenye vyombo vya watumiaji maji vilivyoko katika maeneo yao.END

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA