AJALI MWISHONI MWA MWAKA.
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/12/31/2013 10:39:12 AM
Pamoja na
jitihada mbalimbal;I zinazofanywa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani kupunguza
ajali zisizo na lazima, baadhi ya madereva wameonyesha kupuuza kwa tahadhari
hizo na kusababisha ajali ambazo zinawasababishia vifo au ulemavu.
Mwandishi wa
habari hizi ameshuhudia ajali iliyosababishwa na mwendo wa kasi baada ya gari
ndogo aina ya TOYOTA iliyokuwa inasafiri kati ya Bagamoyo na Mlandizi kuacha
njia na kuvamia vibanda vya wafanyabiashara.
Mwenyekiti
wa serikali ya mtaa Mbwawa, BW.RAMADHAN KONDO amebainisha kuwa gari hiyo iliacha
njia na kugonga vibanda vya wafanyabiashara, na aliyejeruhiwa ni mtu mmoja,
BW.JAFFAR YOHANA ambaye alikimbizwa kituo cha afya Mlandizi.
BW.KONDO
amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.
END.
Comments
Post a Comment