MAMA MISITU YAWAPATIA ELIMU WANANCHI JUU YA UVUNAJI AMAZAO YA MISITU.


Ben Komba/Pwani-Tanzania/10-12-2013

Wananchi wa kijiji Chakenge wamepatiwa elimu maalum kuhusiana na utaratibu mzima unaohusiana na mazao ya misitu kuepusha ukataji holela misitu na  kupunguza malalamiuko kutoka kwa wananchi wa maeneo ya uvunaji.

Akiongea na wanakijiji wa Chakenge, Mratibu wa mradi wa mama misitu msitu wa Ruvu kusini, BW.YAHYA MTONDA amesema kuwa utaratibu wa uvunaji wa mazao ya misitu unaambatana na mambo makuu manne.

BW. MTONDA amefafanua kuwa mambo hayo ni kukata leseni ambayo inatolewa bure, kibali cha halmashauri ambacho kitategemea ujazo wa mazao ya misitu itakayovunwa, kibali cha kusafirisha mazao ya misitu na kibali cha ushuru cha serikali kuu na kibali cha mwenyekiti wa serikali ya mtaa/kijiji.

BW.MTONDA amebainisha kuwa utoaji elimu huo una lengo kuleta mageuzi chanya  katika suala uwajibikaji wa jamii ili kuwajenga katika kutambua umuhimu wa utunzaji misitu na kufahamu taratibu  zinazohusiana na utunzaji wa misitu.

Aidha amewataka viongozi wa vijiji na kamati za maliasili kusimamia kwa makini utunzaji wa misitu asili inayozunguka vijiji vyao kwa kufuata utaratibu mpya ambao wamepatiwa katika kupambana na uvunaji holela wa mazao ya misitu.

END.

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA