MGOGORO USHIRIKA WA CHAURU.
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/12/3/2013 11:52:32 AM
Wanaushirika
wa shamba la umwagiliaji CHAURU Ruvu wilaya ya Bagamoyo katika mkoa wa Pwani,
wameendelea kuwalalamikia maofisa wanaohusika na masuala ya ushirika kutoka
hatua stahili panapotokea migogoro katika ushirika.
Hivi
karibuni mwandishi wa habari hizi amebahatika kuzuru katika ushirika wa umwagiliaji
CHAURU na kukutana na baadhi ya wanachama wa ushirika huo na kubahatika kuongea
na Mkulimwa mwasisi wa ushirika huo, BW.DAUD KINDAMBA ambaye amesema mambo
yanayoendelea katika ushirika huo hayastahili kufumbiwa macho na maofisa
ushirika.
BW.KINDAMBA
amesema yeye shamba lake lipo mfereji namba nne, toka kufika kwa katika eneo
hilo shamba hilo ambalo mwanzo lilikuwa chini ya Wachina na baadaye kukabidhiwa
kwa wazawa baada ya Wachina kuondoka na kukabidhiwa kila kitu kilichokuwepo
eneo hilo.
Ameshauri mamlaka
ya ushirika kuwasaidia wanachama wa ushirika huo kwa vitendo vinavyofanywa na
mtu mmoja na huku wanachama wakiendelea kulalamika kutoridhishwa na uongozi
uliopo ambao umekuwa hauwahusishi katika maamuzi nyeti yanayohusu ushirika huo.
Ambapo wamebainisha
mpaka sasa hawajui utaratibu uliotumika kukodisha harvester machine, kuuziwa
wachina maghala ambayo yalikuwa yanatumika na wakulima ambao ni wanachama wa
ushirika huo kuhifadhi mpunga mara kipindi cha mavuno kinapowadia.
Nikiongea na
mwenyekiti wa Ushirika huo, BW.ZAHOR SENG’ENGE amesema anachofanya sasa ni
kujaribu kutekeleza majukumu yake kwa kutumia staili ya matokeo makubwa sasa,
kuhusu kero za wanachama wa ushirika huo anategemea kuandaa mkutano ambao utatoa
fursa ya kila mtu kuelezea kero na kuzipatia ufumbuzi kwa lengo la kujenga.
END.
Comments
Post a Comment