AKADEMI YA SOKA YA AMAZON MKURANGA



Ben Komba/Pwani-Tanzania/10-12-2013/11:20

Akademi ya mchezo ya mchezo wa  soka ya AMAZON iliyopo katika halmashauri ya wilaya ya Mkuranga imeanzisha mashindano maalum ya umri wa miaka 17 na 14 kwa lengo ya kuvitambua viapaji vinagli vichanga.

Mkurugenzi wa akademi ya soka ya AMAZON, SHUKURU NGWESHANI amesema mashindano hayo yatatumika kutambua na kukuza vipaji vya vijana ambao watakaoonyesha uwezo wa kusakata kabumbu kwa kiwango kinachostahili.

NGWESHANI amesema mashindano hayo yatashirikisha timu nane, ambapo timu nane kati ya hizo nne zitakuwa za vijana chini ya miaka 14 na nne nyingine chini ya miaka 17.

Aidha NGWESHANI amewaomba wadau wa mchezo wa soka wilayani Mkuranga na Mkoa wa Pwani kuunga mkono hatua ambazo ameaanza kuchukua kupitia akademi ya AMAZON katika suala zima la kuibua vipaji.

END.

Comments

Popular posts from this blog

MAFUNZO YA UREFA