TAARIFA YA UTEKELEZAJI JESHI LA POLISI PWANI
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/12/26/2013 9:41:12 AM
Takwimu za
Jeshi la Polisi mkoa wa Pwani zimebainisha kuwa katika kipindi cha mwaka 2013,
jumla ya matukio 3705 yameripotiwa katika vituo mbalimbali vya Polisi, kati ya
makosa hayo ni Mauaji, Kubaka, Kulawiti, Wizi wa watoto na utupaji wa watoto.
Akisoma
taarifa ya utekelezaji ya Jeshi hilo katika mkoa wa Pwani, Kamishna msaidizi
mwandamizi, URLICH MATEI amebainisha kuwa makosa hayo yamegawiwa katika makundi
manne, makosa dhidi ya ubinadamu, makosa dhidi ya kuwania mali, Makosa dhidi ya
maadili ya jamii na makosa ya usalama barabarani.
Kamanda
MATEI amezungumzia upande wa makosa ya
kuwania mali ambayo yametokea katika kipindi cha mwaka 2013 ni pamoja na
kukamatwa kwa noti bandia zenye thamani ya milioni 3,040,000/= huko Chalinze
katika wilaya ya Bagamoyo ambazo zilikuwa zimehifadhiwa ndani ya bahasha.
Kwa upande
wa uhalifu dhidi ya maadili ya jamii, Kamanda MATEI ameongeza kuiwa Jeshi la
Polisi limeweza kudhibiti maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Pwani kwa kufanya misako
na kufanikiwa kukamata wahamiaji haramu kutoka ETHIOPIA na Somalia.
Aidha katika
kipindi hicho wilayani Kisarawe katika eneo la Kauzeni kata ya Vikumburu ,
Jeshi la Polisi lilifanikiwa kukamata vipande 70 vya meno ya Tembo kwenye
kizuizi cha ukaguzi wa mazao ya misitu na kuwakamata watuhumiwa 9 kati yao 2
wakiwa askari wa Jeshi la Polisi mkoa wa Kinondoni.
Kamanda wa
Polisi mkoa wa Pwani, Kamishna msaidizi
mwandamizi ULRICH MATEI amewaasa madereva kuwa makini wanapoendesha magari
katika kipindi hiki cha sikukuu kutokana na kuwepo kwa shamrashamra
zinazoambatana nazo.
END.
Comments
Post a Comment