MWIZI MTANDAONI ATUPWA JELA MIAKA 10.
Ben Komba/Pwani-Tanzania/04/25/2013/5:34:57 PM Mkazi wa mtaa wa Mwendapole, BW. CHARLES BEATUS maarufu kwa jina la Ngoge amehukumiwa kwenda jela miaka 10 kwa kosa la wizi katika mtandao pamoja na wizi wa kuaminiwa. Akisoma hukumu hiyo hakimu mkazi wa Kibaha BI.HERRIETH MWAILOLO mtuhumiwa ametiwa hatiani baada ya mahakama kujiridhisha na ushahidi uliotolewa na kufanya mtuhumiwa huyo kuingizwa hatiani na kuhukumiwa kifungo cha miaka 10 jela. Inadaiwa kuwa tarehe 05 May 2011, BW. GWELINO WILFRED mkazi wa Kongowe wilaya ya Kibaha aligundua kuibiwa kutoka akaunti yake kiasi cha shilingi milioni moja laki tatu na themanini-3,380000/= kutoka katika akaunti yake katika Tawi la NMB Mjini Kibaha yenye namba 2121606490 ambapo fedha zake zilihamishwa kupitia mtandao wa NMB-MOBILE kupitia namba yasimu 0767-122144 na kuhamishiwa kwenye akaunti yenye namba 2031614880 inayotumiwa na mtuhumiwa huyo. Kesi hiyo iliyokuwa inasimamiwa na wakili wa serikali BW. SALIM MSEMO mtuhumiwa BW. CHARLES B...