VIDEO-WANAWAKE WAGWAYA KUGOMBEA MAJIMBONI WAKIMBILIA VITI MAALUM.
Ben Komba/Pwani-Kibaha/7/24/2015 12:02:11 PM Hali ya wanawake kuwa nyuma katika kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali za uwakilishi imejitokeza kwa kiasi kikubwa katika mchakato wa kuwatafuta wagombea ambao watawakilisha vyama vyao katika uchaguzi mkuu ujao unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu. Kati ya wagombea wa nafasi ya udiwani kata ya Tumbi mjini Kibaha, Angalau mwanamama NURU MSADALA MAGEGE ameamua kujitokeza kupambana kuhakikisha ile asilimia hamsini kwa hamsini ya uwakilishi inafikiwa. BIBI.NURU MSADALA MAGEGE ambaye alikuwa kivutio kwa wana ccm ambao wamehudhuria mkutano huo, kwa kuweza kujieleza kwa ufasaha akiwa ni mwanamke pekee kati ya wagombea wanane ambao wote ni wanaume. Amewaahidi wana CCM ambao wamehudhuria mkutano huo wa kampeni za ndani kwa ndani za chama katika Kata ya Tumbi, Tarafa ya Kibaha mjini Kibaha kuwa atahakikisha anasimamia majukumu yake ya kuwakilisha wananchi kwa uaminifu mkubwa ili kuweza kuwaletea maendeleo endelevu wan...