WACHIMBA MCHANGA MJINI KIBAHA WALALAMIKA-VIDEO
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/2/6/2015 4:38:19 AM
Wakazi wa
mtaa wa Miyomboni katika halmashauri ya mji wa Kibaha wamejikuta katika wakati
mgumu baada ya halmashauri kuwakabidhi wawekezaji wakubwa shughuli ya uchimbaji
mchanga katika eneo lao na wao wakikosa shughuli ya kuwaingizia kipato.
Mmoja wa wachimba
mchanga ambaye nimebahatika kuongea naye, BW.NOEL KITIMBWISI amesema kuwa kwa
muda mrefu wakazi wa eneo hilo wamekuwa wakitumia machimbo hayo kama ajira
binafsi na kuwawezesha kujikimu na changamoto mbalimbali za maisha.
BW.KITIMBWISI
ameitaka halmashauri ya mji kuangalia haki za wachimbaji wadogowadogo badaala
ya kutotoa fursa kwa kundi hilo kubwa ambalo lina vijana wengi na kinamama
ambao wamejiajiri katika sekta hiyo ya uchimbaji wa madini ya mchanga.
Ambapo
kinamama wanafaidika kwa kupika mamalishe na kujipatia riziki, lakini hali
imebadilika toka mwekezaji huyo alipofika eneo hilo bila wao kushirikishwa na
kuleta kijiko ambacho kwa njia moja au nyingie imeathiri kwa kiasi kikubwa
kipato cha wenyeji.
Naye BI.WEMA
MFAUME mama lishe katika eneo hilo amesema leo ni siku ya pili wamekuwa
wakipata hasara kutokana na wachimba mchanga wadogowadogo ambao walikuwa
wanawategemea kama wateja wao wakubwa kushindwa kununua chakula kutoka kwao
kutokana na mabadiliko ghafla yaliyojitokeza.
BI.MFAUME
amebainisha kuwa ni vyema serikali ikaliangalia vizuri suala la wawekezaji kwa
kuweka sheria ambazo zitawalinda wenyeji w eneo husika, ili kutoa fursa kwa
kila mtu kula kwa urefu wa kamaba yake.
Naye
mwekezaji anayelalamikiwa, BI.AGNES FRANK amesema kuwa yeye amekodisha eneo
hilo kwa madhumuni ya kuchimba mchanga na kuuza kwa wenye malori na hatua ya
wachimbaji wadogo kuzuia magari kuingia machimbo kuchukua mchanga ni kitu cha
kushangaza.
BI.AGNES
FRANK ameongeza yeye ana vibali vyote vya uchimbaji wa madini hayo ya mchanga,
na katika kurahisisha utendaji wake amekodisha kjiko ambacho kinamgharimu
shilingi milioni 1.2 kwa siku, kitu ambacho wachimbaji wadogowadogo hawakitaki
katakata.
Mpaka
mwandishi wa Habari hizi anaondoka eneo la tukio maaskari kadhaa walioshika
bastola na Bunduki kutoka kituo cha Polisi Mlandizi walikuwa wanarandaranda
kulinda hali ya usalama ili hali ikisemekana kuna wachimbaji wawili wamekamatwa
na wanashikiliwa na Polisi.
END
Comments
Post a Comment