JAMII YAPASWA KUSAIDIA WATOTO.
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/2/9/2015 10:59:31 AM
Jamii
imeagizwa kuzingatia utunzaji wa watoto wanaoishi katika mazingira magumu ili kuweza kuto fursa kwa watoto wenye
wazazi na wasio na wazazi kupata elimu na mahitaji muhimu.
Mjumbe wa
halmashauri kuu ya CCM kutoka mkoa wa Pwani, BW.RUGEMALIRA RUTATINA amesema
hayo wakati wa kukabidhi misaada kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu
katika maeneo ya Kibaha, Kwa Mfipa ambao umetolewa na kikundi cha kuweka na
kukopa cha UPENDO.
BW.RUGEMALIRA
amesema ni juu ya jamii kuweka mikakati madhubuti ya kuwasaidia watoto ambao
hawana usaidizi katika masuala mbalimbali ili kuweza kuwaokoa na majanga
mbalimbali ya kidunia kutokana tu, na kukosa usimamizi na ilihali wakiishi na
jamii yenye kujua kwa undani tatizo hilo.
Naye msoma
risala wa kikundi cha Kuweka na kukopa cha UPENDO, BIBI.FATMA TEA amesema
kikundi chao kwa kuona umuhimu wa watoto wanaoishi katika mazingira magumu kwa
makusudi walianzisha fungu kwa ajili ya kuwasaidia watoto yatima na wanaoishi
katika mazingira magumu.
BIBI.TEA
ameongeza fungu hilo kuwasaidia watoto yatima na wanaoishi katika mazingira
magumu linatumika kuwasaidia watoto hao inapotokea wamepatwa na dharura ya
maradhi, ada ,vifaa vya shule na mahitaji mengine yanayojitokeza kwa mwanadamu.
Wamewataka
wanajamii wengine kuiga mfano wa kikundi chao wa kuanzisha fungu maalum ambalo
kila mwanachama inampasa kuchangia shilingi mia tano kila wanapokutana ili
kuwasaidia watoto wenye uhitaji.END
Comments
Post a Comment