HATIMAYE SHULE INAYOONGOZA KWA UCHAKAVU HALMASHAURI YA MJI KIBAHA YAANGUKA.
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/2/3/2015 2:22:30 AM
Hatimaye
shule ya msingi Mailimoja ilyopo katikati ya halmashauri ya mji wa Kibaha
hatimaye imeanguka kufuatia malalamiko ya muda mrefu ya walimu,wanafunzi na
wazazi wa kutaka halmashauri ya mji wa Kibaha kuchukua hatua za haraka kunusuru
majengo ya shule hiyo.
Mwandishi wa
Habari hizi amefika katika shule hiyo na kushuhudia paa la moja ya majengo
ambalo limekuwa linatumika kwa ajili ya darasa kati ya madarasa manne ambayo
wanatumia kati ya madarasa 11 na shule yenye wanafunzi 1080.
Mwalimu mkuu
wa shule hiyo, MWL.REGINALD FANUEL amesema hiyo ndiyo hali halisi ambayo ipo
shuleni hapo na kwa sasa wanapanga mikakati ya kukabiliana na hali hiyo na
wakitegemea halmashauri ya mji wa Kibaha kufanya makubwa zaidi katika
kuhakikisha shule hiyo inakuwa eneo salama la kufundisha na kujifunzia.
BW.FANUEL
ameongeza mara baada ya kuanguka paa la jingo hilo ndipo Mkurugenzi mtendaji wa
halmashauri ya mji wa Kibaha, BI.JENIFA OMOLO amezuru eneo hilo na kumtaka
mkutano na wazazi ili kuja kupanga kwa pamoja hatua ambazo zitachukuliwa.
END,
Comments
Post a Comment