MADAWA YA KULEVYA KILO NNE YAKAMATWA PWANI
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/2/28/2015
Jeshi la
Polisi Mkoani Pwani umekamata kilo nne za unga unaosadikiwa kuwa madawa ya
kulevya katika maeneo ya Kibaha kwa Mathias, katika halmashauri ya mji wa
Kibaha.
Kwa mujibu
wa mashuhuda wa tukio hilo ambao hawakutaka majina yao kutajwa kuhofia usalama
wao, Mmoja wao amebainisha kuwa unga huo ulikamatwa majira ya saa tatu usiku
kufuatia msako wa kumatafuta mtuhumiwa KANONI KAFU KANONI ambaye amekiuka
masharti ya dhamana ya kesi mbalimbali zinazomkabili.
Baada ya
Polisi kufika katika eneo la tukio wakiongozwa na Afisa upelelezi ALLY MASIMIKE
kutoka kituo cha Polisi cha Tumbi, mtuhumiwa katika mazingira yasiyoeleweka
alifanikiwa kukimbia na kuwaachia Polisi na wadhamini waliotega mtego wa
kumkamata nyumba.
Na ndipo
kufuatia hali hiyo ndipo Polisi wakaanza kufanya upekuzi na kufanikiwa kupata
BRIEF CASE ambayo ilikuwa na unga kilo nne, na waligundua unga huo walipofika
kituoni Tumbi na kufungua mbele ya walalamikaji ambao walimdhamini BW.KANONI
KAFU KANONI katika tuhuma nyingine zinazomkabili.
Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Pwani Mrakibu mwandamizi
msaidizi ULRICH MATEI amethibitisha kutokea tukio hilo tarehe Februari 20 mwaka
huu majira ya saa tatu usiku.
Mwandishi wa
Habari hizi alipotaka kujua hatua gani itafuata baada ya madawa hayo kukamatwa
siku tisa zilizopita mpaka sasa,Kamanda MATEI amesema unga huo unatarajiwa
kupelekwa kwa mkemia mkuu wa serikali wakti wowte kuanzia sasa.
Comments
Post a Comment