SUMATRA YAKAGUA MABASI YA ABIRIA
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/2/8/2015 12:09:53 PM
Mamlaka ya
udhibiti ya usafarishaji waangani na nchi kavu-SUMATRA-imefanya zoezi la
ukaguzi magari yanayosafirisha abiria katika kuhakikisha maderva wote wanakuwa
na leseni na kukagua uzima chombo cha usafiri.
Msemaji wa
SUMATRA, BW.DAVID MZIRAY amesema zoezi hhilo wameliendesha kwa pamoja na Jeshi
la Polisi ili kuto matokeo yaliyo bora na katika kuhakikisha sheria na taratibu
za usafirishaji ambazo zimewekwa na SUMATRA zinafuatwa kikamilifu.
Moja ya
taratibu ambazo zimepewa kipaumbele ambayo wenye magari ya kusafirisha abiria
wanakiuka mara zote ni upandishaji wa nauli kunakofanywa na mawakala wao kwa
makusudi na hivyo kumnyonya abiria.
BW.MZIRAY
amesisistiza ukaguzi huo utaendelea kufanyika mara kwa mara ili kuwezesha
kupunguza kero wanazokumbana nazo wasafiri hususan suala hilo la kupandisha
nauli kiholela kwa wananchi.
END.
Comments
Post a Comment