WABABA WAASWA KUACHA KUNYEMELEA WANAFUNZI WA KIKE
Ben Komba/Pwani-Tanzania
Naibu mkuruigenzi
elimu ya sekondari, TAMISEMI, BI.PAUKLINE NKWAMA amewataka wadau mbalimbali
kujitokeza katika kuhakikisha watoto wa kike wanapatiwa nafai ya kujiendeleza
kielimu ili kuweza kuwakwamua na changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo.
BI.NKWAMA
ameyazungumzia hayo wakati wa kikao cha Mkutano mkuu wa kiwilaya wa shirika
lisilo la kiserikali linalosaidia katika utoaji usaidizi kwa watoto wa kike
wanaokabiliwa na changamoto mbalimbali za kimaishala CAMFED.
BI.NKWAMA
ameongeza lengo la wadau kukutana kama walivyokutana hapo ni kujaribu kutambua
changamoto mbalimbali zinazowakabili na kujitokeza katika upatikanaji wa elimu
kwa watoto wa kike wanaoishi katika mazingira magumu ili waweze kupata
maendeleo binafsi na familia zao.
Amewataka wanafunzi
wanaopatiwa usaidizi na shirika hilo la CAMFED {CAMPAIGN FOR FEMALE EDUCATION}
kutumia msaada huo wa kielimu katika kuhakikisha wanajiendeleza zaidi katika
suala zima la kuwa na maisha yenye mafanikio baadaye.
Aidha,
BIBI.NKWAMA alitumia fursa hiyo kukemea tabia ya baadhi ya kinababa watu wazima
kuwatongoza wanafunzi wa kike kwa kutumia vishawishi mbailimbali na hivyo
kuwaharibia mustakabali wa maisha yao ya baadaye.
Mkurugenzi wa
CAMFED Tanzania, BI.LYDIA WILBARD amesema shirika lao linafanya kazi kwa kutoa
kipaumbele kwa mtoto wa kike katika kuhakikisha wanatengeneza mazingira rafiki
yatakayomuwezesha mtoto wa kike kupata elimu ambayo wanaamini itamsaidia katika
maisha yake ya baadaye.
BIBI.WILBARD
amebainisha kuwa katika utekelezaji wa mpango huo wamekuwa wakikabiliwa na
changamoto mbalimbali ikiwemo suala la utoro,mombam zisizotarajiwa, matumizi
mabaya ya fedha zinazotolewa kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi, ufaulu mdogo na
kukosekana kwa ushirikiana kutoka kwa wazazi katika suala zima la kusimamia
maendeleo ya mtoto wa kike hususan katika masuala ya elimu.
END
Comments
Post a Comment