RIDHIWAN ATAKA WANANCHI KUZINGATIA AMANI
<>
|
<>
RIDHIWAN AHIMIZA AMANI KIPINDI CHA UCHAGUZI
Ben Komba/Pwani-Tanzania
Mjumbe wa halmashauri kuu ya Taifa ya CCM, BW.RIDHIWAN KIKWETE amewataka wapiga kura katika Jimbo la Chalinze kuwa watulivu kipindi chote cha mchakato wa uchaguzi wa serikali za mitaa, vitongoji na vijiji. Ameyazungumza hayo wakati akiongea na halmashauri ya Jimbo la uchaguzi Chalinze CCM, BW. KIKWETE amesema ni jambo bora kwa wananchi kuhudhuria katika mikutano ya kampeni ili kupata fursa ya kupima sera za kila chama. BW. KIKWETE amewaambia wajumbe wa kikao hicho kuwa mpaka sasa CCM kimepita katika nafasi 301 bila kupingwa na hivyo kujihakikishia ushindi wa kishindo katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Desemba 14 nchi nzima. Hata hivyo BW.KIKWETE amesema kuna baadhi ya maeneo katika Jimbo la uchagui la CHALINZE hayataweza kushiriki uchagizi huo kutokana na sababu mbalimbali akizitaja kuwa ni Chamakweza na Pongwe mnazi kutokana na sababu mbalimbali zilizojitokeza. Naye Katibu mkuu msaidizi wa Idara ya oganaizesheni ya CCM, BW.STEVEN KAZIDI amesema kwa upande wao harakati zinaendelea kwa utulivu pamoja na kujitokeza kwa kasoro ndogondogo ambazo zinaweza kufanyiwa kazi kama walivyokubaliana walipokutana viongozi wote wa vyama vya siasa walipokutana na TAMISEMI. END |
Comments
Post a Comment