ALA NJAMA KUUA
12-Dec-14
12:22:35 AM-Tanzania/
Katika hali
inayoashiria kuwa Dunia ya sasa imani imekwisha, wakazi wawili wa kijiji cha
Soga halmashauri ya wilaya ya Kibaha wameokoka kutoka katika mteggo wa kuuwawa
kutokana na kuwa tishio kwa maharamia wa ardhi katika kijiji hicho.
Mmoja wa
watu waliotaka kuuwawa ambaye ni Meneja
wa shamba la ALAVI ESTATE linalomilikiwa na MOHAMED ENTERPRISES amesema kuwa
alipata taarifa kutoka kwa Mkuu wa kituo kidogo cha Polisi Kongowe na kuelezwa
kuwa kuna watu wanakula njama ya kutaka kumuua.
Bw.AMIR
ameongeza kuwa sababu kubwa ambayo ilitaka kugharimu maisha yake ni mmoja wa
maharamia wa mashamba, BW.RAMADHAN RASHID ambaye amejipata yupo katika kibano
kufuatia kujishuhulisha na uuzaji wa mashamba ya ALAVI ESTATE, na hivyo ili kuficha uvundo huo ndipo alipokula njama
ya kukodi watu kuwauwa ambao anaona ni kikwazo katika azima yake hiyo.
Naye mtu
mwingine ambaye alikuwa kati ya watu waliotakiwa kuuwawa mgombea wa nafasi ya
Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Soga aliyejulikana kwa jina moja BW.LIAMBA
amesema kuwa yeye kilichomponza ni kutanaza sera zake wakati wa kushawishi
uchaguzi wa ndani wa chama kuahidi kuwashuhulikia watu ambao wamejihusisha
kuuza ardhi kinyume cha taratibu.
Kutokana na
kauli yake hiyo ilionekana kumkera,BW.RAMADHAN RASHID ambaye naye alikuwa
anaombea nafasi hiyo kupitia mchakato wa ndani wa CCM na kushindwa na BW.LIAMBA, Hali ambyo
haikumpendeza mtuhumiwa huyo.
BW.LIAMBA
amebainisha kuwa kutokana na hilo, Mtuhumiwa alienda eneo la Kongowe na
kukodisha watu ambao wangetekeleza mpango huo, ambao kwa njia moja au nyinine
hawakukubaliana na mpano huo na hivyo kwenda kutoa taarifa Polisi na kufanikiwa
kuweka mtego ambao ulifanikiwa kumtia hatiani mtuhumiwa huyo, ambaye baadaye
aliachiwa katika mazingira ya kutatanisha hali ambayo inawaachia mazingira
maumu wakazi wa kijiji cha Soga.
END.
Comments
Post a Comment