MKUU WA MKOA WA PWANI ATAKA BARABARA ZITUNZWE
Ben
Komba/Pwani-Tanzania/desemba 4 2014
Mkuu wa mkoa
w Pwani,BI.MWANTUMU MAHIZA ameitaka wakala wa barabara mkoani hapa kuhakikisha
wanaweka vibao kuainisha vivuko kwa ajili ya binadamu mifugo na uzito wa magari
yanayotakiwa kupita njia husika.
BIBI.MAHIZA
amesema hayo katika Kikao cha Bodi ya barabara cha mkoa wa Pwani chenye lengo
la kutathimini maendeleo ya miundombinu ya barabara, ambapo amesema kutokuwepo
na vibao vinavyoashiria magari ya uzito gani yanatakiwa kupita barabara gani.
Mkuu huyo wa
Mkoa amebainisha kwa kutozingatia utaratibu huo wa kuonyesha uzito wa magari
yanayotakiwa kupita njia husika badala ya kufuata utaratibu wa kuhakikisha
limebeba mzigo wa aina gani, ndio chanzo kikubwa cha uharibifu wa barabara
zetu.
Ametoa mfano
wa Barabara ya lami ambayo imejengwa hivi karibuni na halmashauri ya mji wa
Kibaha ambayo kwa sasa inaharibika kwa kasi kutrokana na magari yaliyozidi
uzito kupita katikabarabara hiyo na kusasbabisha baadhi ya maeneo kubonyea na
kuathiri ubora wa barabara.
Na katika hatua nyingine Mkuu wa mkoa wa
Pwani, BIBI.MWANTUMU MAHIZA wataalamu wa masuala ya vivuko TEMESA kuhakikisha
wanafanya jitihada za hali na mali katika kuhakikisha kunapatikana kivuko cha
uhakika katika Mto Rufiji ili kuondoa kero ya usafiri inayowakabili wakazi wa
halmashauri hiyo.
Naye Mkurugenzi
wa TEMESA mkoa wa Pwani, MHANDISI JULIUS HUMBE amesema kuwa wao kwa upande wao
wanafanya jitihada kwa kuwasiliana na wizara kuomba wapatiwe hata boti ndogo za
kubweba abiria 25 ili kupunguza makali ya tatizo.
END.
Comments
Post a Comment