Ben Komba/Pwani-Tanzania/01-3-2014:11:51 Zahanati ya Mkoani inafanyiwa upanuzi kuwezesha kuchukua kinamama wajawazito wapatao 250 mpaka 300 kwa mwezi na ujenzi huo unatarajia kutumia shilingi Milioni 250 ikiwa ni mapato ya ndani ya halmashauri ya mji wa Kibaha. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Mganga mkuu wa halmashauri ya mji wa Kibaha, BW.ISSA KANIKI amesema kuwa Zahanati ya Mkoani imekuwa na tatizo kubwa linapokuja suala la kinamama wajawazito, ambapo kwa sasa Zahanati ina vitanda vya kujifungulia kinamama wajawazito. BW.KANIKI ameongeza ujenzi huoo utawanufaisha zaidi kinamama na watoto wachanga, Mpaka sasa mkandarasi ameshapatikana na ujenzi unatarajia kukamilika Mei 30, moja ya majengo yatakayojengwa ni holi la kupumzikia, holi la kinamama ambao wamejifungua na wanaporudi nyumbani wanapata matatizo na kulazimika kurudi hospitali. aidha amefafanua kuwa kila kitu kimekamilika na hakuna tatizo lolote na mkandarasi yupo eneo ...