NYUKI MKOMBOZI KIUCHUMI
Ben Komba/Pwani-Tanzania/29-11-2013/10:41 Taasisi wa masuala ya haki za binadamu na maendeleo WAHABIMA wanuia kusaidia wajasiriamali wa mjini wa Kibaha katika suala zima la ufugaji wa nyuki wa asali ili kuongeza kipato cha familia. Akizungumza katika uzinduzi wa warsha inayohusiana na ufugaji nyuki wa asali, Mshauri mwelekezi, BW.DOMINIC KIWELE amewaeleza washiriki kuwa ufugaji wa nyuki ukifanywa kwa kuzingatia ushauri wa kitaalamu unaweza kukikomboa familia na umaskini wa kipato ambao ndio tatizo kubwa miongoni mwetu. BW.KIWELE amebainisha kuwa gharama za kuanzisha ufugaji wa nyuki ni ndogo kulinganisha na ufugaji mwingine wowote kwani ili kuweza kufuga nyuki itakubidi kuingia gharama kidogo kwa ajili ya kutengenezea mzinga ambao utatumika kutegea nyuki ukiwa na chambo chake ambacho ni nta inayozalishwa na nyuki. Mshauri mwelekezi huyo, BW.DOMINIC KIWELE amefafanua kuwa watu wengi wamekuwa wanaogopa kufuga nyuki wakihofiwa kushambuliwa nao kitu ambacho sio lo...