MAENDELEO YAHIMIZWA PWANI.
MAENDELEO YAHIMIZWA PWANI. Ben Komba/Pwani-Tanzania/17-09-2013/10:58 Mkuu wa Mkoa wa Pwani,BIBI.MWANTUMU MAHIZA amekemea tabia ya watendaji kusababisha migogoro ya ardhi katika jamii kutokana na utendaji wao kuongozwa na maslahi binafsi hali ambayo inatishia hali ya ulinzi na usalama nchini. BIBI.MAHIZA amewaambia watendaji katika kikao cha kuhimiza maendeleo ya Mkoa wa Pwani kilichofanyika mjini Kibaha kuwa wanachoponzwa nacho ni tamaa ya vifedha vidogo vidogo wanavyopokea ndio kichocheo cha uvinjifu wa amani katika wilaya, Kata na Mitaa/vijiji. BIBI.MAHIZA ameonya kuwa iwapo atabaini viongozi ndio wanahusika katika kuchonganisha raia, basi atahakikisha mhusika anachukuliwa hatua za kisheria bila kujali yeye ni chama gani au ni nani ili kuendeleza utamaduni wa kutii sheria bila shuruti. Amewachukulia watu wanaowachonganisha wananchi katika masuala ni wabaya ambao wanasababisha uvinjifu wa amani. Akiongea katika kikao hicho Mwenyekiti wa serikali Mko...