Posts

Showing posts from June, 2013

Amka Mtanzania: LOWASSA AMTAKA OBAMA ASIZUNGUMIE MAMBO YA USHOGA N...

<a href="http://amka-mtanzania.blogspot.com/2013/06/lowassa-amtaka-obama-asizungumie-mambo.html?spref=bl">Amka Mtanzania: LOWASSA AMTAKA OBAMA ASIZUNGUMIE MAMBO YA USHOGA N...</a>: Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo yaNje na Ushirikiano wa Kimataifa, Edward Lowassa, amemtahadhalisha kujiepusha na kauli za kuunga mkono us...

SIASA YAWAKWAMISHA WADAU WA MAENDELEO

Ben Komba/Pwani-Tanzania Suala la wananchi kusaidiana na serikali katika utekelezaji wa mipango mbalimbali ya maendeleo imeingiliwa na sintofahamu kutokana na baadhi ya wawakilishi wa wananchi kuwa na mawazo potofu kuhusiana na misaada inayotolewa na wadau wa maendeleo wa maeneo yao na nje. Mwandishi wa habari hizi ameshuhudia kujitokeza kwa hali hiyo kayika Kata ya Ubena, ambapo mwananchi mfugaji wa Kimang’ati, BW.ALMAS MGUSA aliyetoa msaada wa mbao, misumari na mifuko ya udongo ulaya kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa baadhi ya majengo muhimu katika shule ya Msingi Tukamisasa. Akitoa msaada huo, BW.MGUSA amesema yeye ametoa msaada huo kwa ajili ya kuisaidia jamii ya hapo na hasa ikizingatiwa kuwa yeye mwenye ni mkazi wa muda mrefu wa eneo hilo la Ubena wilaya ya Bagamoyo. Amesema hatua hiyo ya kutoa misaada kwa shule ya msingi Tukamisasa inafuatia ombi la mwenyekiti wake wa kijiji wa kuomba msaada kutoka kwa wafadhili ili kukamilisha ujenzi wa darasa moja na amebaini...

WATENDAJI WAONYWA KUHUSU UZEMBE

Ben Komba/Pwani-Tanzania/10:40/29-06-2013 Mkuu wa Mkoa wa Pwani BIBI. MWANTUMU MAHIZA amewaonya watendaji katika halmashauri ya wilaya ya Kibaha kufanya kazi kwa bidii na uwajibikaji kuepuka kuwajibishwa na serikali. Akizungumza katika kikao maalum cha baraza la madiwani halmashauri ya wilaya Kibaha, BIBI.MAHIZA amebainisha kuwa wakati wa kuoneana aibu umepita na kila mtu atawajibika kwa uzembe ambao ataufanya. Mkuu wa mkoa wa Pwani , BIBI.MAHIZA alianza kwa kuwaonya watendaji hususan wa ardhi ambao wamekuwa ndio chanzo kikubwa cha migogoro na wanapohamishwa wanaacha malumbano ambayo hayana tija ambayo mengine yanatishia kusumbua hali ya amani na utulivu uliopo. BIBI.MAHIZA ameelezea na kuchukizwa kwake na mgogoro unaoendelea katika kijiji cha Kisabi ambapo maofisa ardhi kwa makusudi wamepima viwanja katika maeneo ya watu bila kuwashirikisha wamiliki wa maeneo hayo, ambapo kuna maeneo yameuzwa kwa watu zaidi ya sita, jambo ambalo amesema halikubaliki. Kutokana na k...

RASIMU YA KATIBA NA MAPUNGUFU

Ben Komba/Pwani-Tanzania/18-06-2013 Kuna mambo ambayo yamejitokeza katika rasimu ya Katiba ilitolewa na Tume ya mabadiliko ya Katiba, ambayo yasipotazamwa kwa umakini yanaweza kulisababishia Taifa vurugu na kuhatarisha usalama wan chi. Akizungumza na mwandishi wa habari  wa habari hizi, Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la YOUTH PARTNERSHIP COUNTRYWIDE lenye maskani yake mjini Kibaha ambaye pia ni Makamu mwenyekiti wa jukwaa la katiba, BW.ISRAEL ILUNDE amesema kuna mapungufu takriban 50. BW.ILUNDE amesema katika rasimu hiyo ambayo imependwa na wananchi wa kada mbalimbali ambayo kwa kiasi kikubwa imezingatia hisia za wananchi kwa kuweza kuyapa nafasi masuala ambayo yalikuwa yamependekezwa na wananchi waliotoa maoni. BW. ILUNDE amefafanua kuwa kwa rasimu hiyo kutoa kipaumbele kwa suala la haki za binadamu limeleta faraja kwa wananchi wengi hasa ikizingatiwa sehemu yenye kufuata misingi ya haki za binadamu basi maendeleo lazima, kwani kutakuwa hakuna kundi am...

NHIF COAST.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/12:19/17-06-2013 Mfuko wa Bima ya afya Taifa una mpango wa kuhakikisha unashughulikia kero zote zinazowakabili wanachama wake zinashughulikiwa ili kufikia malengo ambayo imejiwekea wa kutoa huduma sthahili kwa wanachama wa mfuko huo. Mkurugenzi mtendaji wa mfuko wa Bima ya afya wa Taifa, BW. EMMANUEL HUMBA ameyaongea hayo katika kikao maalum kilichowakutanisha wakuu wa wilaya na watendaji wengine wa mkoa wa Pwani. BW.HUMBA amesema kwa kuanzia watapeleka madaktari bingwa kwa ajili ya wilaya ya Mafia ili kuweza kwenda kutoa huduma kwa wanachama wao wanaosihi na kufanya kazi wilayani humo kutokana na wanachama wao kukabiliwa na tatizo la usafiri wa uhakika. BW. HUMBA amefafanua kuwa kwa wanachama wa mfuko huo wanaosihi Mafia gharama zote za huduma watakazopatiwa zitabebwa na mfuko wa Bima ya afya, wakati wananchi wa kawaida itawalazimu kulipia uchangiaji wa huduma ya afya kama ilivyopangwa na halmashauri au mkoa. Ameongeza madaktari bingwa h...

AKINAMAMA WASAIDIWA MITAJI NA MKE WA MBUNGE KIBAHA MJINI.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/11:59/14-06-2013 Wanawake katika kata ya Kibaha wameshauriwa kuhakikisha wanailinda amani ya nchi yetu kwa kutumia uwezo wao kuhakikisha kuwa amani na utulivu unadumu ili kuweza kupata maendeleo endelevu. Katibu wa Jumuiya ya wazazi mjini Kibaha, BI.MWATABU HUSSEIN amebainisha kuwa kinamama wao ndio wana jukumu la kuhakikisha wanasimamia heshima na maadili ya Taifa. BI.HUSSEIN amesema amani ya Tanzania inapotezwa na watoto zao au waume zao kutokana na vitendo wanavyofanya ambavyo vinaweza kuhatarisha amani kwa kushauri au kukemea tabia zinazojitokeza katika ngazi ya awali, na watakao taabika yatakapotokea majanga ya vita ni kinamama, watoto na wazee. Naye Mke Mbunge wa Kibaha mjini, BIBI SELINA KOKA ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo ya kukutana wanawake ambao wamejiajiri katika sekta isiyo rasmi amesema amejiwekea utaratibu endelevu wa kuwafikia kinamama kila kata ili kuwaamsha wafanye shughuli za uzalishaji mali. BIBI.KOKA kati...

VIJANA WAJITOLEA KUREKEBISHA MIUNDOMBINU.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/08/06/2013/15:08 Katika hatua inayoonyesha vijana sasa wanatambua majukumu na wajibu wao katika jamii, wamejiunga na kuanzisha kikundi cha kujitolea katika kata ya Mailimoja mjini Kibaha katika suala zima la kuboresha miundombinu katika eneo wanaloishi. Mmoja wa vijana ambaye nimeongea naye BW. IMANI CHANGAMOTO wakiwa katikati ya shughuli hiyo ya kusawazisha miundombinu ya barabara ya maeneo yao ya kwa SHEKHE MUDHIHIR kutokana na kuharibika vibaya katika kipindi cha mvua zilizopita. BW. CHANGAMOTO amebainisha kuwa kitu kikubwa ambacho kimewafanya wao kujitolea kuziba mashimo maeneo yao ni kutokana na kujihadhari na dharura ambayo inaweza kujitokeza, hususan kuugua ghafla na majanga mengine ya asili ambayo yanatokea bila taarifa ilihali miundombinu ikiwa mibovu. Naye Mwenyekiti wa Kikundi hicho cha NYOTA NJEMA, BW. MANSOOR LIPAMBILA amesema eneo ambalo lilikuwa korofi zaidi ni karibu ya hospitali ambako kulikuwepo na mahandaki ambayo yalikuwa in...

SUMATRA WANYOOSHA MSTARI.

Ben Komba/Pwani-Tanzania/08/06/2013/13:32 Watanzania wametakiwa kutoa ushirikiano stahili kwa SUMATRA wanapokuwa safarini ili kuweza kupunguziwa kero zinazowapata wanapokuwa wanasafiri kuelekea maeneo mbalimbali ya Tanzania. Afisa mfawidhi mkuu wa SUMATRA mkoa wa Pwani, BW.NASHON IROGA amesema hayo alipozungumza na mwandishi wa habari hizi kufuatia uwepo wa kampeni maalumu ya ukaguzi wa mabasi inayoendeshwa katika kituo kikuu cha mabasi mjini Kibaha. BW.IROGA amebainisha kuwa operesheni hiyo inayoendeshwa sambamba na askari wa usalama barabarani, na lengo kubwa la mamlaka hiyo ni kuhakikisha wanadhibiti vitendo vyote vya mabasi ya abiria kukatisha ruti,kutototoa tiketi kwa abiria na mengine. Amefafafanua kuwa kuna changamoto mbalimbali zinazojitokeza ambazo nyingi zinasababishwa na madereva kukiuka taratibu za usafirishaji kwa makusudi kutokana na kuzongwa na tama, akitoa mfano wa mabasi yanayofanya safari za Ubungo mpaka Mlandizi, ambayo nyakati za jioni yanaishia M...

PWANI YAPANIA KUFUNGUA NDONDI,MAELFU WAFURIKA KUMUAGA MANGWEA,CCM YASIMAMISHA VIONGOZI BAGAMOYO

Ben Komba/Pwani-Tanzania/06/06/2013/12:12 Mkoa wa Pwani katika halmashauri ya mji wa Kibaha kumeanzishwa rasmi kampeni ya kuinua mchezo wa ngumi ambao unaonekana kuwa na wapenzi wengi mjini na kubainika uwepo wa vipaji wa mchezo huo kwa vijana wengi wa mjini hapa. Kocha wa mchezo huo anayetambuliwa na chama cha olimpiki ulimwenguni, BW. GAUDENCE UYAGA amebainisha hayo baada ya kufanya mahojiano na mwandishi wa habari hizi kando ya Mazoezi ya mabondia anaowafundisha. BW. UYAGA amesema kuwa mchezo huo umekuwa hukikosa udhamini kutoka kwa wafadhili kutokana na wengi kukosa msukumo wa kujua ni wapi wanaweza kupata wachezaji wa mchezo huo, na kukatishwa tamaa na baadhi ya watu wanaojifanya mapromota ilihali wakitanguliza mbele maslahi yao binafsi na kusahau haki za mabondia wanaowachezesha. BW.UYAGA ametoa mfano kuwa kuandaa pambano moja la ngumi , Bondia inampasa kukaa kambini si chini ya miezi mitatu na katika  muda huo bondia anahitajika kutumia si chini ya shilingi ...