MGOGORO STENDI
Ben Komba/Pwani-Tanzania/27-May-13/19:42:08 Sakata kubwa limeibuka kufuatia amri ya kuwataka wafanyabiashara wanaotoa huduma ya kutoa na kupokea fedha kwa njia ya simu za mkononi sawa na wauza vocha na wafanyabiashara wengine kuondoa vibanda vyao vya biashara katika eneo hilo. Kamera ya SIBUKA TV imeshuhudia wafanyabiashara hao wakimsongasonga mmoja wa wanamgambo wa halmashauri ya mji kwa kiklichodaiwa kupita na kuandika vibanda vyao kutumia rangi ya mafuta ya kupuliza neno ondoka hali iliyozua ghadhabu kiasi cha kukaribia kumuadhibu mgambo huyo. Mazingira ya watu wanaofanya shughuli zao kutokubaliana hatua ya Mgambo hao kupita wakiandika kila kitu kilicho mbele yao, ONDOA hali iliyozua taharuki miongoni mwa wafanyabiashara hao ambao wanadai wanafuata taratibu zote za kisheria kuwepo katika eneo hilo. Akiongea kuhusu tujkio hilo la mgambo wa halmashauri kupita kuandika katika maeneo mbalimbali ya vibandavya stendi, Bwana afya wa Kata ya Mailimoja, BW. ABUBAKAR SHAH amesema ...