CHANJO MPYA YA NIMONIA NA ROTAVIRUS WANACHI WAHAMASISHWA.
Ben Komba/Pwani-Tanzania/30-Nov-12/06:27:06 Wananchi wilayani Kibaha wametakiwa kuto ushirikiano wa kutosha kwa watoa huduma ya chanjo ROTAVIRUS na NIMONIA katika suala zima la uimarishaji wa afya, na katika muda wote wa utekelezaji wa zoezi hilo ambalo likifanikiwa litawezesha kufanya magonjwa ya uti wa mgongo na kuharisha kwa watoto wadogo kuwa historia hapo baadaye. Akizungumza katika kikao cha uhamasishaji na kamati ya afya ya msingi ya wilaya, Mwakilishi wa mkuu wa wilaya Bw. ANATOLY MHANGO amekemea tabia ya baadhi ya watu kupotosha malengo ya chanjo mbalimbali zinazotolewa kwa jamii katika kuiepusha na magonjwa ambayo yanaweza kukingika. BW. MHANGO amewaasa wananchi kutoa ushirikiano ili kuweza kiampeni hiyo ya chanjo ya RITOVIRUS na NIMONIA ifanikiwe, katika kuhakikisha suala zima la kuboresha huduma ya afya ya jamii. Naye Mratibu wa chanjo halmashauri ya wilaya ya Kibaha, BIBI. REHEMA PILIMO amesema kuwa ROTAVIRUS ni vimelea vinavyosababisha kuharisha kwa watoto...